Inonga anaondoka Simba mwishoni wa msimu huu 2024

Pole sana mtani, huu mwaka mbali duuuh, huku timu mbovu, kule wachezaji wanataka kusema, pale umepigwa FA yaani mtani huna raha kabisa mwaka huu.
 
Waondoke tu hakuna tatizo...

Kimsingi Inonga hana faida yeyote akiwa Simba, hujituma akiwa national team...

Malone yeye ndiyo kiazi kabisa, aondoke hata sasa hivi tu.
Yaani ukuta wa Yericko leo hii kawa kiazi? Kweli wapenzi wa Simba ni wanafiki
 
Unaumwa bawasili sio bure Kisinda yupo RS Berkane wapo nusu fainali federation, Mukoko yupo nusu fainali na Mazembe, Msuva haina haja ya kueleza , Feisal anapambania kiatu, Saido yupo hapo kwenu nani kawaloga hao? nitajie wachezaji 5 waliofanikiwa baada ya kutoka 5imba
 
Uzuri Simba hatunaga bifu na wachezaji wakimaliza wanaondoka kwa amani au wanauzwa,au kutolewa kwa mkopo kwa amani bila kelele...sio huko ubuntu botho ..weee
Halogwi wala nini Simba wanajua kuachwa. Hakuna atakaemshobokea ili baadae ije kuwa bifu. Afuate utaratibu aende.
 
ok sawa
 
Kimsingi Inonga hana faida yeyote akiwa Simba, hujituma akiwa national team...
Hii kauli nimeisikia wanasimba wengi wakiisema ila nadhani ina kasoro. Kwa maoni yangu national team wamejua madhaifu ya Inonga na wamemuelekeza jinsi ya kucheza ili yasiidhuru timu kitu ambacho Simba hakijafanyika.

Kwa mfano, Inonga siyo mzuri katika kupiga pasi ndefu, yaani 95% ya pasi zake ndefu nyingi zinapotea na nyingi kati ya hizo unajiuliza aliona nini hadi anazipiga maana mpira unaenda mahali ambapo hakuna mchezaji mwenzake. Inawezekana ana mapungufu ya macho kuona mbali. Kwa pungufu hili ukiangalia alivyocheza AFCON, Inonga alikuwa hapigi pasi ndefu, na mara nyingi walikuwa hata hawamchezeshi mpira. Kazi yake ilikuwa kukaba na kuzuia, akipata mpira anaachia kwa mtu wake wa karibu anarudi kwenye jukumu lake la msingi, uchezaji tofauti na ule akiwa Simba.
 
Kwa hali hii Yanga atakuwa bingwa kwa miaka mingi sana. Maana wapinzani kila mwaka watakuwa wako busy kujenga tu kikosi chao, huku wakiendelea kujipa matumaini kupitia yule msemaji mwenye damu ya Kinjekitile Ngwale, mwilini mwake.
Subiri shoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…