kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kuna watu wanamsema Inonga kuwa anafanya makosa mengi uwanjani siku hizi kuliko zamani bila kuangalia mambo muhimu. Ukweli ni kwamba Inonga hana raha kucheza Simba.
Inonga ni mchezaji mkubwa sana, anapata namba kikosi Cha kwanza Cha DRC ambacho kimesheheni wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana wanaocheza ulaya. Wachezaji hawa yawezekana wamemwambia mengi sana kule afcon yanayomvunja moyo kucheza timu kama Simba.
Kucheza kwenye timu ambayo imekosa ubingwa wa ligi kwa misimu 2 mfululizo ingawa yeye anacheza vizuri sana uwanjani inaweza kumvunja moyo wa kupambana.
Kufungwa goli 5 na Yanga inawezekana hakujamuondoka kichwaji.
Rafiki yake Mayelle kulipwa hela nyingi huko aliko pyramids kunaweza kumchanganya akili
Kuumia mara kwa mara kwenye timu ambayo haichukui makombe wala kuvuka robo finali za CAF kunamkatisha tamaa mchezaji anaejituma sana uwanjani.
Inawezekana mchezaji huyu ana uchovu mwingi sana kutokana na kucheza mechi nyingi sana za Simba na za timu ya taifaa, inawezekana ana maumivu mahali.
Hakuna mtu anaekaa na Inonga kumuuliza anapitia shida zipi kabla ya kumlaumu kila Kona mitandaoni.
Dube hakuwa na Raha kwenye timu ambayo anavuja jasho jingi sana na kuumia lakini hanyanyui makwapa yake kushangilia. Hakuna mchezaji anaitwa timu yake ya taifa anaependa kucheza timu isiyoshinda.
Kaeni na Inonga badala ya kumlaumu.