GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ewe ' insect ' uliyopo Tanzania najua fika kuwa tokea uingie mwaka 1981 umekuwa na hasira nasi Wanadamu ila nisikufiche kwa sasa unatuudhi kwani huwachukui Watu kwa mpango ' Maalum ' na kila mara unatushtua tu hasi sasa unatutisha na wengine.
Ewe ' insect ' uliyopo Tanzania kwani huo Udongo bado haujatosheka tu hadi unazidi tu Kutuchukulia Watu wetu muhimu na ambao si Siri ndiyo wanatusaidia Sisi wengineo ' Tegemezi ' kwa Maisha yetu ya hapa na pale?
Ewe ' insect ' uliyopo Tanzania halafu kwanini kila Wazungu hasa Wamarekani, Waingereza na Wacanada wakitaka ' Kukumata ' ili upunguze Kutupelekea Watu wetu muhimu Udongoni huwa unawakwepa na furaha yako ni kuona tu kila uchao Watanzania tunalia na Kuhuzunika?
Ewe ' insect ' uliyopo Tanzania basi Mimi GENTAMYCINE safari hii nakuomba na tena nipo chini ya Miguu yako nakuomba kuanzia sasa kama kweli unataka Watu wa Kuwapeleka Udongoni basi anza na Wanasiasa Waongo Waongo, kisha nenda kwa Wale waliompiga risasi 39 Mbunge mmoja hivi na kama utaona inafaa basi malizia na wale Wanaotupa Miili ya Wenzao Mitoni, Maziwani na Baharini.
Ewe ' insect ' uliyopo Tanzania kusema ukweli Watanzania tumelia sana na sasa nadhani tumechoka Kulia kwani hutupi hata muda wa Kupumzika kututoa Machozi na unaendelea tu Kutuliza huku mwenyewe ukiona raha kwanini lakini? Kwani unavyowapeleka Udongoni hawa Watu wetu muhimu Kimaisha na kutuachia Mingumbaru ( Mijinga ) na Mipopoma ( Mipumbavu ) mingi una maana gani na unategemea nini?
Ewe ' insect ' uliyopo Tanzania sasa ni matuamini yangu kuwa uliyemchukua leo au uliowachukua Wiki moja iliyopita na hata Mwezi hao hao watakuwa wamekutosha na sasa umeshiba kama siyo Kuridhika hivyo kuanzia sasa utatuacha Watanzania tufurahi na Watu wetu muhimu ambao wamekuwa na Msaada kwa Maisha yetu na kwamba hutokuja Kutuliza tena kwakuwa wengine hadi hivi sasa Machozi yetu yote yamekauka kabisa kwani tuliyatoa yote kwa Wapendwa wetu.
Nawasilisha.