Inspekta Mwala ahukumiwa mwaka mmoja gerezani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Inspekta Mwala alikuwa akiendesha gari kwenye barabara ya Mazeras kabla ya kusababisha ajali

- Mwala ametakiwa kuitumikia jela kwa mwaka mmoja au kulipa faini ya KSh 30,000

- Kabla ya uamuzi kutolewa na hakimu Adalo, Mwala aliiomba msamaha familia ya marehemu na kusema hakutenda kosa kwa kukusudia

- Familia ya Mangi ilisema kuwa itarejea mahakamani kumshurutisha Mwala kuwalipa fidia

Mcheshi Davis Mwabili almaarufu Inspekta Mwala, ametakiwa kulipa faini ya KSh 30,000 au kufungwa jela kwa mwaka mmoja baada ya kupatikana na kosa la kusababisha ajali kwa kuendesha gari kiholela

Uamuuzi huo ulifanywa Alhamisi, Septemba 19 na hakimu mkazi wa mahakama ya Mariakani Nelly C. Adalo.

Mahakama iliarifiwa kwamba Agosti 26, 2019 mida ya saa tatu usiku akiendesha gari lenye usajili wa KCV 807C kwenye barabara ya Kaloleni kuelekea Mazeras, Mwala alisababisha ajali akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake kabla ya kumgonga na kumuua Ismael Mangi.
Upasuaji wa maiti ya Mangi uliofanywa katika hospitali ya Coast General ulionesha kwamba marehemu alifariki kutokana na majeraha mabaya ya kichwani baada ya kugongwa.

Kabla ya hakimu kumsomea hukumu, Mwala aliiomba msamaha familia ya Mangi na kusema kuwa hakukusudia kuyakatiza maisha ya mwanao kwenye ajali hiyo.
"Pole. Naomba msamaha kwa familia ya marehemu. Sikukusudia kuisabaisha ajali hiyo. Sikukusudia kuua," Mwala alisema.
Kwenye umauzi wake, hakimu Adalo alisema kuwa aliutilia maanani msamaha wa Mwala ambaye pia alikuwa amekiri makosa yake na hivyo basi akaagiza afiungwe jela kwa mwaka mmoja au atozwe faini ya KSh 30,000.
Hata hivyo, familia ya Mangi ilisema kuwa itarejea mahakamani kumshurutisha Mwala kuwalipa fidia kufuatia kifo cha mwanao.
 
Mwala si mkenya huyo au mnazungumzia mwala wa wapi? Ma afisa uhamiaji fuatilieni hili jina.
 
Mwala alikuwa yule wa akina mama kayaii, mzee ojwang et al. Huyu anayejifanya askari sio kabisa
 


Ndiyo si huwa anajifanya Inspector wa polisi, sasa kakumbwa na mainspector halisi wa polisi. Pole sana Insp, Mwala.🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…