Instagram Ads

sometimesyes

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2017
Posts
360
Reaction score
288
Habari bandugu

Nina biashara yangu nataka kutangaza Instagram kupitia zile 'Sponsored Ads' nimejaribu kutafuta msaada Google bila mafanikio, mwenye uelewa au uzoefu jinsi inavofanyika naomba msaada kwny uzi huu tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kutangaza Instagram kwa kutumia ads hauendi direct instagram, kuna kitu kinaitwa "facebook business" hapa ni maalum kwa matagazo kwenye FB na insta kwa kutumia ads..
-nenda google search 'facebook business'
-chagua compose new ads
-itakuletea form ya kujaza kipengele cha kwanza ni 'audience' na cha pili ni 'budget'
-AUDIENCE hapa changua tagazo lako lionekane wapi eg locanition:TANZANIA, state: DSM, AGE: 18>64
-BUDGET hapa una chagua unalipia kiasi gani na kwa namna ipi
unaweza kulipia tangazo lako kwa namna zifuatazo
CPC
CPM
CPA
hapa kila njia inagarama yake
-ukisha malika kuna kitu ninaitwa FB auction hapa utachagua tangazo lako lipatikane wapi Eg. Fb, insta au kote kwa pamoja
Nb: garama inategemea aina ya tagazo na malipo ni USD
>Nipo busy kidogo mkuu saiv, kama nikipata mda nitakuelewesha hizo CPC, CPM na CPA,
 
Mkuu rudi uje umalizie.
 

Rudi umalizie


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutengeneza matangazo ya facebook ni njia bora katika kupata wateja kwa urahisi zaidi na kwasasa unapoweka tangazo lako linaonekana kote yaani instagram na Facebook pia.

Kuna vitu vya msingi ambavyo ni vema kujua kabla ya kutengeneza tangazo lako.

Jua aina ya wateja unaowataka. Jua sifa ya wateja unaowataka, elimu, umri, sehemu unazolenga tangazo lako kufikia na interest zingine pia.

Wengi sometimes huwa wanafanya makosa kwa kuweka matangazo hayo bila kuangalia hizo sifa wakati wa kutengeneza tangazo hilo, ni vema kucheza na takwimu za kimtandao facebook (Audience Insight) ili kuweza kutengeneza tangazo ambalo litafikia wateja ambao watanunua bidhaa yako na siyo kuishia kupata likes na comments ambazo kiujumla hazitoweza kukuletea wateja walio na nia ya kununua bidhaa au huduma yako.

Hivyo ni bahadhi ya vitu vya msingi vya kuelewa ili tangazo lako liweze kukusaidia kutimiza nia yako ya kupata wateja.

Kama kutakuwa na yeyote ambaye anagependa kujifunza hatua kwa hatua namna ya kutengeneza hayo matangazo na kutumia Audience insight tools kwaajili ya kutarget wahusika wako tunaweza wasiliana PM.

Pia kwa wale ambao wangependa kupata huduma ya kutengenezewa hayo matangazo pia huduma inapatikana. Tuwasiliane PM kwa uhitaji zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…