Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,240
App ya Instagram inaweka sehemu mpya ambayo itawezesha watumiaji kurekebisha ujumbe wa DM.
Kwa sasa Instagram haina sehemu ya kurekebisha (edit) ujumbe katika sehemu ya DM. Endapo kama ukituma ujumbe, utaona hakuna sehemu ya ku-edit, sehemu ambayo ipo ni "unsend" ambayo inafuta ujumbe ambao umekosea kuutuma.
Mabadiliko mapya yatawezesha sehemu ya ku-edit message ambayo mtumiaji amekosea kuituma.Watumiaji wa Instagram wanalazimika kufuta message ambayo wameikosea na kuandika upya au kuandika ujumbe wa kurekebisha message ambayo imekosewa.