Instagram kuwalazimisha wateja wanaojisajili kuandika umri wao kwaajili ya usalama wa watoto

Instagram kuwalazimisha wateja wanaojisajili kuandika umri wao kwaajili ya usalama wa watoto

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Sasisho jipya la Instagram linawataka wote wanaojiunga na mtandao huo wa kijamii kuandika umri wao, vinginevyo hawataweza kujiunga na mtandao huo.

Hatua hiyo mpya ya Instagram haitawaathiri wote ambao wamekwishajisajili kwenye mtandao huo, lakini itawalenga wateja wapya wanaojisajili, ikiwa na lengo la kuwazuia watu wenye umri chini ya miaka 13 kujiunga na mtandao huo.

“Hatukuwa na ulazima wa kuwauliza watu umri wao kihistoria, kwa kuwa tulitaka Instagram kuwa sehemu ambayo watu wanaweza kujieleza kwa uhuru bila kujali uhalisia wao,” taarifa ya blogu Instagram ilieleza, ikiongeza kuwa haitaonesha taarifa hizo katika akaunti za watumiaji.

Mtandao huo umejitetea kuwa taarifa za umri wa watumiaji utasaidia kuwaweka salama watumiaji wenye umri mdogo na kuwasaidia kupata mahitaji kulingana na umri wao.

Hatua hiyo imepingwa vikali na Watetezi wa Haki za Watumiaji wa Mitandao wakisema kuwa inakiuka Sheria za Faragha ya Watoto Mtandaoni za Marekani (US Child Online Privacy Protection Act) ambayo inazuia makampuni yote ya teknolojia kukusanya taarifa za mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 13.

Watetezi hao wameilaumu kampuni ya Facebook kwa kukiuka sheria hiyo kwa muda mrefu, ikiendelea kukusanya taarifa za watumiaji wenye chini ya umri wa miaka 13.

Utafiti uliofanyika mwaka 2018 ulionesha kuwa zaidi ya nusu ya makosa ya uhalifu wa kingono mtandaoni yamefanyika katika mitandao inayomilikiwa na Facebook, yaani Facebook, Instagram na WhatsApp, ikihusisha zaidi ya visa 4,000 vya kusambaza picha za watoto mitandaoni.

Chanzo: Independent
 
Back
Top Bottom