INSTINCTS ARE MATHEMATICAL / MACHALE NI MAHESABU :: From my personal experience as a Data Engineer and Computer Programmer

kali linux

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,192
Reaction score
5,685
Hello bosses........

Nadhan hii inawakuta watu wengi pia. Kuna muda unafanya decision bila kuwa na sababu yoyote ya msingi au logical. Hii wazungu hupenda kuiita 'gut feeling'. Yaan unaweza panga kwenda safari lakini ghafla tu unaamua kuahirisha halafu unasikia basi ulilopanga kusafiria limepata ajali. Au unajikuta tu unawaza kwenda sehemu fln na huko unaenda kukutana na bonge la bahati au dili la kazi. Hio fikra inayokusukuma kufanya kitu kinachokuletea manufaa bila kuwa na sababu yyt ya msingi waswahili tunaiita 'Machale' na kwa kizungu wanaita 'Instinct'

Sasa kwa muda mrefu nimekua nasoma makala nyingi kuhusiana na namna binadamu anavyofanya maamuzi na ni drives gani zinamsukuma mtu kufanya hayo maamuzi. Nikaja kugundua kwamba hayo yote yanaelezwa kwa kutumia principles za hesabu. Na ndipo nikaishia kukubali msemo fln unasema "INSTINCTS ARE MATHEMATICAL"

---> TUJIKUMBUSHE HILI KWANZA KUHUSU NAMNA BINADAMU ANAVYOFANYA MAAMUZI.
Maamuzi yote yanayofanya na binadamu ni lazima yapitie kwenye mfumo wa fahamu (Muunganiko wa Sensory organs, Nerves, Brain au Spinal Cord). Na hayo maamuzi yote binadamu anaweza kuyafanya akiwa kwenye state hizi tatu:-
1. CONSCIOUS (AKIWA NA FAHAMU)
2. SUB-CONSCIOUS (AKIWA NA NUSU FAHAMU)
3 UN-CONSCIOUS (AKIWA HANA FAHAMU)

Maamuzi mtu anayofanya akiwa na ufahamu kamili nadhan tunayafahamu, na yale akiwa hana kabisa ufahamu nadhan tunayafahamu pia (mfano kujigeuzageuza ukiwa umelala fofofo etc....). Mimi leo niko interested na haya maamuzi ambayo mtu anafanya au yale matendo ambayo mtu yanampata akiwa Sub-conscious.

Kuwa sub-conscious haimaanisha kuwa hujitambui. Mfano unaweza kuwa unakimbia na focus yako yoye ipo kwenye kukimbia lakini ni kawaida ya ubongo kuprocess information zozote zinazokuzunguka. So ubongo unaweza kuwa unafanya kazi subconsciously lakini ww focus yako ipo kwenye kukimbia tu, hili naomba lieleweke kwa sababu ndio kiini cha kitu nnachotaka kuzungumzia leo.

----> UHUSIANO ULIOPO KATI YA COMPUTER NA HUMAN BRAIN (AT DESIGN AND OPERATIONAL LEVEL)
Ubongo wa binadamu ni machine moja complex sana kuanzia namna inavyojifunza na namna inavyotunza data au taarifa mbalimbali na kuziprocess. And trust me maboresho yote watu wanayoyafanya kwenye computers na hizi all in one chips zime-base kwenye kuiga 'mimicing' namna ubongo unavyofanya kazi. Mambo kama Random Access Memory, Read only memory, data processing etc... yote yalikua inspired kutokana na ufanyaji kazi wa 'Human Brain', Ubongo

Sasa baada ya field ya computer science kukua watafiti baadhi wakaanza kujiuliza kwa nini hii machine (computer) tuloitengeneza na kuifanya iweze kukumbuka na kuprocess data tusiifanye iweze kujifunza kutokana na hizo data inazoziona? Na hicho ndicho kilichokua kimebaki katika harakati za kuiga namna ubongo unavyofanya kazi. Hillo swali ndilo limezalisha field za Machine Learning na Artificial Intelligence. Na field zote hzo deep down ni mahesabu ya ajabu sana kuwahi kufanywa kwenye ulimwengu huu ukiachana na yale ya Einstein na Nikola Tesla (Much respect).

Ubongo unajifunza kutokana na data inazopokea kutoka kwenye sensory organs. Ubongo wa mtoto mdg aliozaliwa tunaweza sema unakua empty coz hauna experience yyt. Mtoto akishika moto akaungua anajua hii haifai, na hio ni kwa sababu ubongo wake unajifunza kutokana na hicho kitendo na madhara yake. Hi ndio tunaiita 'Learning' kwa kimalikia (RIP). So tunaweza sema mtu anajifunza kutokana na experience lkn hio inategemea uwezo wa ubongo wake kujifunza. Hii inathibitishwa na mambo mbalimbali, mfano waswahili tunasema 'UTU UZIMA DAWA' Hii ni kwasababu mtu mzima anakua amepitia experiences nyingi hivo ubongo wake unakua umejifunza mambo mengi.

Na watafiti walivyoona hivo basi wakaamua kutengeneza hii field ya 'MACHINE LEARNING', ambayo lengo lake ni kufanya Machine (Computer) Iweze kujifunza kupitia Data Au Experience (tukilinganisha na ubongo). Na hii ufanyika kwa kupitisha Data nyingi sana kwenye algorithms mbalimbali ambazo hutafuta pattern na kisha kutengeneza models ambazo ndizo hutumika kufanya future decisions. Somo kuhusu undani wa hio kitu na process zake ni issue ya kuongelea siku nyingine. Leo naongelea namna Machale/ Instincts zinavyotengenezwa.

----> INSTINCTS / MACHALE (ZI)YANATENGENEZWAJE NDANI YA UBONGO? NA HESABU INAHUSIKANAJE HAPO?
Kama upo na mm hadi hapa basi nadhan umesoma nlivoelezea namna Machine Learning Inavofanyika. Kwa kurudia tu ni kwamba Data(Past experience) zinapitishwa kwenye 'Algorithms' (Mathematical decision making processes), Kisha hizo Algorithms hutumia very complex maths kugundua PATTERNS zilizopo ndani ya hizo data. Kisha hizo 'PATTERNS' hutumika kutengeneza MODELS ambazo hutumiwa na computer kufanya decision au kubashiri output in the future. Mfano computer inaweza pewa data za picha za wanawake thn inatengeneza patterns na kutumia hizo patterns kutengeneza model. Baadae computer itapewa picha random (ambayo haikuwepo awali) na kuulizwa ibashiri kama ni mwanamke au mwanamme. Sasa quality ya jibu inategemea na quality ya data zilizotumika wakati wa learning, hii iko hvohvo pia kwenye maisha yetu.

Kama umenielewa hapo juu basi process hiohio ndio hutumiwa na ubongo wa mwanadamu kutengeneza Machale/Instincts. Wewe ukiwa unafanya mambo yako mengine basi ubongo huwa unalearn 'sub-consciously' kutokana na mazingira uliopo, mambo unayosikia, vitu unavyofanya, vitu unavyoongea kwa kukurupuka na effect zake etc..... kisha ubongo wako unatumia hesabu zake kichwani kucreate pattern na kutengeneza decision making models ambazo sasa next time ukiwa unahitaji kufanya maamuzi fln na upo kwenye mazingira yanayofanana na your past experience (kpnd ubongo una-learn subconsciously bila ww kujua) hizo models zinakua-triggered na unajikuta unaamua tu bila kufikiria. Sasa ufasaha wa maamuzi hayo yanatokana na quality pamoja na quantity ya experience zako. Unaweza fanya maamuzi kwa machale na ukapata matokeo mabaya coz data/experience yako haitoshi lkn kwa wale wanaopata matokeo mazuri basi utakuta experience yao kwenye hilo jambo / field ni kubwa kiasi. Lakini hio learning yote inafanywa ww ukiwa hauna focus kwenye hilo jambo wakati huo na ndio maana wataalam wanaiita 'SUB-CONSCIOUS LEARNING', na kwa kuwa ww haukuwa na habari kpnd unajifunza(actually kpnd ubongo wako unajifunza) basi utaona ni bahati na kuita machale/instinct.

Hio haina tofauti sana na unaposhika kitu cha moto ukaungua then next time unaamua usikishike tena (CONSCIOUS LEARNING) kwa kuwa umejifunza, tofauti pekee ni kwamba kwenye kujenga instincts unakuwa umejifunza bila wewe kujua (SUB-CONSCIOUS LEARNING).

Ni hayo tu bosses, anyway kwa mwenye tatizo lolote ambalo anapenda kutatua kwa ufasaha zaidi kutumia Machine Learning, Artificial Intelligence au Data Analysis iwe kwenye biashara, product design, financial trading, etc...... anaweza kunitafuta tufanye kazi.

Peace.........
~ kali linux
 
Kama binadamu ni mashine, basi ni the most advanced, complicated machine kwenye hii dunia.
Nashangaa sana watu wanaosema comp ina akili kuliko binadamu.
We make billions of calculations everyday bila hata kujua tunafanya hesabu. Niliwahi kuona wanatengeneza robot likawa lilisha glass na vitu laini vinavunja na kuharibu.
Lakini binadamu mkono wake umajua hiki kitu ni laini, faster ubongo usjacalculate pressure utakayotumia kukishika yani unavyoshika kitu soft kama andazi ni tofauti na unavyoshika chuma.
Unapovuka barabara unapiga hesabu haraka kujua speed ya gari muda itakapofika ulipo, distance ya kutoka ulipo mpaka upande wa pili, utembee kwa speed gan uvuke beforw garo kufika yote within seconds.
 
Na ndio lengo la researchers kwenye field za Artificial Intelligence na Robotics kufikia huko. Kuna projects kama Robot 'Sophia' zinaonesha maendeleo mazuri kwenye hio sector
 
Kama binadamu ni mashine, basi ni the most advanced, complicated machine kwenye hii dunia.
Nashangaa sana watu wanaosema comp ina akili kuliko binadamu.
We make billions of calculations everyday bila hata kujua tunafanya hesabu. Niliwahi kuona wanatengeneza robot likawa lilisha glass na vitu laini vinavunja na kuharibu.
Lakini binadamu mkono wake umajua hiki kitu ni laini, faster ubongo usjacalculate pressure utakayotumia kukishika yani unavyoshika kitu soft kama andazi ni tofauti na unavyoshika chuma.
Unapovuka barabara unapiga hesabu haraka kujua speed ya gari muda itakapofika ulipo, distance ya kutoka ulipo mpaka upande wa pili, utembee kwa speed gan uvuke beforw garo kufika yote within seconds.
Asante mkuu leo nimejifunza kitu kipya ambacho nimekuwa nikikifanya katika maisha yangu yote bila kujua kama ninakifanya.

buccaneer Tazama mawazo ya great thinkers haya.
 
Hio iko wazi hakuna kitu Cha ajabu kama ubongo wa binadamu unafanya kazi 24/7 na unatumia umeme mdogo sana yaan energy efficiency ya ubongo ni fumbo gumu sana

Hapo ujaongelea neurons ambazo zipo billion 86 mpaka 100 ziko connected
 
Kama binadamu ni mashine, basi ni the most advanced, complicated machine kwenye hii dunia.
Nashangaa sana watu wanaosema comp ina akili kuliko binadamu.
Kuna summit ilifanyika china elon na jack ma walukua wangumzaji wakubwa (main speaker) elon aligoma kabisa kuamini kwamba sisiwatu ni smart kuliko computer. Nilipenda presentation ya jack ma sema ilikua na mapungufu
We make billions of calculations everyday bila hata kujua tunafanya hesabu. Niliwahi kuona wanatengeneza robot likawa lilisha glass na vitu laini vinavunja na kuharibu.
Lakini binadamu mkono wake umajua hiki kitu ni laini, faster ubongo usjacalculate pressure utakayotumia kukishika yani unavyoshika kitu soft kama andazi ni tofauti na unavyoshika chuma.
Nadhani kwenye robotics bado hatujawa advance sana. Labda tusubir robot za tesla. Lkn kwenya kazi wa wiwandani robotics zimesaidia sana ku cut cost.
Unapovuka barabara unapiga hesabu haraka kujua speed ya gari muda itakapofika ulipo, distance ya kutoka ulipo mpaka upande wa pili, utembee kwa speed gan uvuke beforw garo kufika yote within seconds.
Hili tatizo lili ikita uber. Uber bhana alitengeze gari lao. System yao ilikosea calculation za speed ambayo mtu anatuma kuvuka barabara na speed ya gari. Baada ya hii ajali uber waka suspected project yao ya self driving
 
Kuna summit ilifanyika china elon na jack ma walukua wangumzaji wakubwa (main speaker) elon aligoma kabisa kuamini kwamba sisiwatu ni smart kuliko computer. Nilipenda presentation ya jack ma sema ilikua na mapungufu
Jack Ma aliongea lkn kiukweli alikua hana point nzr zaidi ya elon. Na isitoshe jack ma alikua anatumia maneno mabaya, pia elon alikua anamset kisha jack ma anaingia kingi mwenyewe hadi watu wanacheka. Anyway, kwa mtazamo wangu elon alikua sahihi hasahasa point yake kuhusu speed of execution ya hizi computer. Alisema "To a computer, 1 second is an eternity but to human beings it's nothing" Hio statement ina maana kubwa sana. Ukiachana na smartness ya hz systems ukaongelea speed ndipo utaona hatari zaidi ambayo akili kubwa kama elon wanaiogopa
 
Kuna summit ilifanyika china elon na jack ma walukua wangumzaji wakubwa (main speaker) elon aligoma kabisa kuamini kwamba sisiwatu ni smart kuliko computer. Nilipenda presentation ya jack ma sema ilikua na mapungufu

Nadhani kwenye robotics bado hatujawa advance sana. Labda tusubir robot za tesla. Lkn kwenya kazi wa wiwandani robotics zimesaidia sana ku cut cost.

Hili tatizo lili ikita uber. Uber bhana alitengeze gari lao. System yao ilikosea calculation za speed ambayo mtu anatuma kuvuka barabara na speed ya gari. Baada ya hii ajali uber waka suspected project yao ya self driving
Nakuhakikishia ni ngumu robotics kuwa na cognitive abilities kubwa Zaid ya ubungo wa binadamu
 
Kuhusiana na AI
Kuba baadhi ya sector niliziona kwa africa kama ni developer unaeeza kutengeneza mkwanja
1. Kwenye kilimo
- hapa unaweza tengeneza model itakayo chakata ni ugojwa gani unasumbua ilo zao kwa kupitia picha. Mfano mm nalima miogo nimeenda shambani nimekuta majani ya miogo yangu yamekua ya njano. Nacho fanya ni kipiga picha halafu na upload kwenye app au whatever ambayo ipo powdered na AI iweze kubpredict ni ugonjwa gani na nini soln gani ya kufanya. ( hii nilisha wahi kucomment kwenye uzu wa mkuu mmoja alileta hapa)

2. Health care
- kuna app inatumia video. Yani unafanya kana una recod video kama sec 30 iyo app inakupima pressure, siju stress hani ni zuri. Nimesahau jina kidogo
 
Jack Ma aliongea lkn kiukweli alikua hana point nzr zaidi ya elon. Na isitoshe jack ma alikua anatumia maneno mabaya, pia elon alikua anamset kisha jack ma anaingia kingi mwenyewe hadi watu wanacheka. Anyway, kwa mtazamo wangu elon alikua sahihi hasahasa point yake kuhusu speed of execution ya hizi computer. Alisema "To a computer, 1 second is an eternity but to human beings it's nothing" Hio statement ina maana kubwa sana. Ukiachana na smartness ya hz systems ukaongelea speed ndipo utaona hatari zaidi ambayo akili kubwa kama elon wanaiogopa
Tatizo hizo robotics haziwez fikia uwezo wa ubunifu uliokua nao ubongo
 
Hello bosses........

Nadhan hii inawakuta watu wengi pia. Kuna muda unafanya decision bila kuwa na sababu yoyote ya msingi au logical. Hii wazungu hupenda kuiita 'gut feeling'. Yaan unaweza panga kwenda safari lakini ghafla tu unaamua kuahirisha halafu unasikia basi ulilopanga kusafiria limepata ajali. Au unajikuta tu unawaza kwenda sehemu fln na huko unaenda kukutana na bonge la bahati au dili la kazi. Hio fikra inayokusukuma kufanya kitu kinachokuletea manufaa bila kuwa na sababu yyt ya msingi waswahili tunaiita 'Machale' na kwa kizungu wanaita 'Instinct'

Sasa kwa muda mrefu nimekua nasoma makala nyingi kuhusiana na namna binadamu anavyofanya maamuzi na ni drives gani zinamsukuma mtu kufanya hayo maamuzi. Nikaja kugundua kwamba hayo yote yanaelezwa kwa kutumia principles za hesabu. Na ndipo nikaishia kukubali msemo fln unasema "INSTINCTS ARE MATHEMATICAL"

---> TUJIKUMBUSHE HILI KWANZA KUHUSU NAMNA BINADAMU ANAVYOFANYA MAAMUZI.
Maamuzi yote yanayofanya na binadamu ni lazima yapitie kwenye mfumo wa fahamu (Muunganiko wa Sensory organs, Nerves, Brain au Spinal Cord). Na hayo maamuzi yote binadamu anaweza kuyafanya akiwa kwenye state hizi tatu:-
1. CONSCIOUS (AKIWA NA FAHAMU)
2. SUB-CONSCIOUS (AKIWA NA NUSU FAHAMU)
3 UN-CONSCIOUS (AKIWA HANA FAHAMU)

Maamuzi mtu anayofanya akiwa na ufahamu kamili nadhan tunayafahamu, na yale akiwa hana kabisa ufahamu nadhan tunayafahamu pia (mfano kujigeuzageuza ukiwa umelala fofofo etc....). Mimi leo niko interested na haya maamuzi ambayo mtu anafanya au yale matendo ambayo mtu yanampata akiwa Sub-conscious.

Kuwa sub-conscious haimaanisha kuwa hujitambui. Mfano unaweza kuwa unakimbia na focus yako yoye ipo kwenye kukimbia lakini ni kawaida ya ubongo kuprocess information zozote zinazokuzunguka. So ubongo unaweza kuwa unafanya kazi subconsciously lakini ww focus yako ipo kwenye kukimbia tu, hili naomba lieleweke kwa sababu ndio kiini cha kitu nnachotaka kuzungumzia leo.

----> UHUSIANO ULIOPO KATI YA COMPUTER NA HUMAN BRAIN (AT DESIGN AND OPERATIONAL LEVEL)
Ubongo wa binadamu ni machine moja complex sana kuanzia namna inavyojifunza na namna inavyotunza data au taarifa mbalimbali na kuziprocess. And trust me maboresho yote watu wanayoyafanya kwenye computers na hizi all in one chips zime-base kwenye kuiga 'mimicing' namna ubongo unavyofanya kazi. Mambo kama Random Access Memory, Read only memory, data processing etc... yote yalikua inspired kutokana na ufanyaji kazi wa 'Human Brain', Ubongo

Sasa baada ya field ya computer science kukua watafiti baadhi wakaanza kujiuliza kwa nini hii machine (computer) tuloitengeneza na kuifanya iweze kukumbuka na kuprocess data tusiifanye iweze kujifunza kutokana na hizo data inazoziona? Na hicho ndicho kilichokua kimebaki katika harakati za kuiga namna ubongo unavyofanya kazi. Hillo swali ndilo limezalisha field za Machine Learning na Artificial Intelligence. Na field zote hzo deep down ni mahesabu ya ajabu sana kuwahi kufanywa kwenye ulimwengu huu ukiachana na yale ya Einstein na Nikola Tesla (Much respect).

Ubongo unajifunza kutokana na data inazopokea kutoka kwenye sensory organs. Ubongo wa mtoto mdg aliozaliwa tunaweza sema unakua empty coz hauna experience yyt. Mtoto akishika moto akaungua anajua hii haifai, na hio ni kwa sababu ubongo wake unajifunza kutokana na hicho kitendo na madhara yake. Hi ndio tunaiita 'Learning' kwa kimalikia (RIP). So tunaweza sema mtu anajifunza kutokana na experience lkn hio inategemea uwezo wa ubongo wake kujifunza. Hii inathibitishwa na mambo mbalimbali, mfano waswahili tunasema 'UTU UZIMA DAWA' Hii ni kwasababu mtu mzima anakua amepitia experiences nyingi hivo ubongo wake unakua umejifunza mambo mengi.

Na watafiti walivyoona hivo basi wakaamua kutengeneza hii field ya 'MACHINE LEARNING', ambayo lengo lake ni kufanya Machine (Computer) Iweze kujifunza kupitia Data Au Experience (tukilinganisha na ubongo). Na hii ufanyika kwa kupitisha Data nyingi sana kwenye algorithms mbalimbali ambazo hutafuta pattern na kisha kutengeneza models ambazo ndizo hutumika kufanya future decisions. Somo kuhusu undani wa hio kitu na process zake ni issue ya kuongelea siku nyingine. Leo naongelea namna Machale/ Instincts zinavyotengenezwa.

----> INSTINCTS / MACHALE (ZI)YANATENGENEZWAJE NDANI YA UBONGO? NA HESABU INAHUSIKANAJE HAPO?
Kama upo na mm hadi hapa basi nadhan umesoma nlivoelezea namna Machine Learning Inavofanyika. Kwa kurudia tu ni kwamba Data(Past experience) zinapitishwa kwenye 'Algorithms' (Mathematical decision making processes), Kisha hizo Algorithms hutumia very complex maths kugundua PATTERNS zilizopo ndani ya hizo data. Kisha hizo 'PATTERNS' hutumika kutengeneza MODELS ambazo hutumiwa na computer kufanya decision au kubashiri output in the future. Mfano computer inaweza pewa data za picha za wanawake thn inatengeneza patterns na kutumia hizo patterns kutengeneza model. Baadae computer itapewa picha random (ambayo haikuwepo awali) na kuulizwa ibashiri kama ni mwanamke au mwanamme. Sasa quality ya jibu inategemea na quality ya data zilizotumika wakati wa learning, hii iko hvohvo pia kwenye maisha yetu.

Kama umenielewa hapo juu basi process hiohio ndio hutumiwa na ubongo wa mwanadamu kutengeneza Machale/Instincts. Wewe ukiwa unafanya mambo yako mengine basi ubongo huwa unalearn 'sub-consciously' kutokana na mazingira uliopo, mambo unayosikia, vitu unavyofanya, vitu unavyoongea kwa kukurupuka na effect zake etc..... kisha ubongo wako unatumia hesabu zake kichwani kucreate pattern na kutengeneza decision making models ambazo sasa next time ukiwa unahitaji kufanya maamuzi fln na upo kwenye mazingira yanayofanana na your past experience (kpnd ubongo una-learn subconsciously bila ww kujua) hizo models zinakua-triggered na unajikuta unaamua tu bila kufikiria. Sasa ufasaha wa maamuzi hayo yanatokana na quality pamoja na quantity ya experience zako. Unaweza fanya maamuzi kwa machale na ukapata matokeo mabaya coz data/experience yako haitoshi lkn kwa wale wanaopata matokeo mazuri basi utakuta experience yao kwenye hilo jambo / field ni kubwa kiasi. Lakini hio learning yote inafanywa ww ukiwa hauna focus kwenye hilo jambo wakati huo na ndio maana wataalam wanaiita 'SUB-CONSCIOUS LEARNING', na kwa kuwa ww haukuwa na habari kpnd unajifunza(actually kpnd ubongo wako unajifunza) basi utaona ni bahati na kuita machale/instinct.

Hio haina tofauti sana na unaposhika kitu cha moto ukaungua then next time unaamua usikishike tena (CONSCIOUS LEARNING) kwa kuwa umejifunza, tofauti pekee ni kwamba kwenye kujenga instincts unakuwa umejifunza bila wewe kujua (SUB-CONSCIOUS LEARNING).

Ni hayo tu bosses, anyway kwa mwenye tatizo lolote ambalo anapenda kutatua kwa ufasaha zaidi kutumia Machine Learning, Artificial Intelligence au Data Analysis iwe kwenye biashara, product design, financial trading, etc...... anaweza kunitafuta tufanye kazi.

Peace.........
~ kali linux
Uzi mreeefuuuu mnoooo. Aliyesoma wote na kuelewa tafadhali atufanyie wepesi kwa muhtasari
 
Nakuhakikishia ni ngumu robotics kuwa na cognitive abilities kubwa Zaid ya ubungo wa binadamu
Ni ngumu lakini inawezekana. Miaka 20 ilopita hamna mtu alietabili tech itafika hapa tulipo kwa sasa.

Kuna member mmoja kaongelea debate ya elon na jack ma. Nashauri uiangalie iko youtube, then sikiliza point za elon ndo utaona dunia inapoelekea na elon anakua na hofu sana kuhusu A.I coz speed ya maendeleo kwenye hii field ni kubwa mnoo, na ikiendelea hivo binadamu tutakua out-smarted kwenye kila kitu na hizi computers
 
Uzi mreeefuuuu mnoooo. Aliyesoma wote na kuelewa tafadhali atufanyie wepesi kwa muhtasari
Haahaaaaa Pole mkuu..... ila kiufupi kabisa ni kwamba. Ubongo unafanya calculations na kujifunza 'sub-consciously' bila sisi kujua. Matokeo ya huko kujifunza ndio machale sasa hayo
 
Labda kwa sasa. Miaka 10 to 15 ijayo computer zitakuwa na uwezo mkubwa sana. Ipo siku utaenda hospital uta opt kuhudumiwa na robot kuliko doctor wa koti leupe.
one gram of DNA can store approximately 220,160 terabytes, hapo sijaongelea ubongo yaani uwezo wa ubongo wa kuwa creative, kutumia logic ni kitu ambacho robot kuja kuweza ni ngumu sana

Robot wataweza repetitive task Ila kwenye ubunifu, yaan robot kuwa wabunifu kutawapa ugumu sana
 
Back
Top Bottom