Intaneti imezidi kupanda Bei

Intaneti imezidi kupanda Bei

Internet-Money

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2021
Posts
493
Reaction score
1,135
Jana, nimenunua 640 MB kwa sh. 1000 lakini kuamka asubuhi 350 MB Ni kwa hiyo 1000. Kwa hiyo gharama imepanda mara mbili ndani masaa machache. Yote haya Ni kwa sababu upinzani wa Rais upo mtandaoni.

Hili balaa lilianza Baada ya huyu Rais kuingia madaraki. Kutokana na kusemwa sana akaanza kupandisha virushi.

Enzi za Magufuli kwa sh. 500 unapata 1GB - 500 mb , na alisisitiza sana taasi za serikali kuhamia mtandaoni.
Hii ilichangia ongezeko la internet users.

Madhara ya kupunguza watumiaji wa intaneti Ni makubwa :-

Kuwa na lundo la wasomi wasioendana na kasi ya duniani (wasomi wa vitabu).
Uhaba wa ma-programmer
Mifumo itakuwa ni analog
Hivi Leo Kuna watu ni matajiri kutokana tu na kucheza game online, (Ninja).
 
Jana, nimenunua 640 MB kwa sh. 1000 lakini kuamka asubuhi 350 MB Ni kwa hiyo 1000. Kwa hiyo gharama imepanda mara mbili ndani masaa machache...
Hapo sijui tuseme nani anaupiga mwingi kati ya
1. Waziri wa habari
2. TCRA
3. Kampuni za Mawasiliano
4. Watumiaji wa mitandao
 
Kusema kweli bei zimeenda juu sana wakati walikuwa wanajinadi kwamba mkongo wa taifa ukikamilika internet itakuwa sawa na bure na blah blah nyingine, nchi zilizoendelea internet ni hitaji la msingi, huku ndo tunazidi kuongezeana tozo.......
 
Tatizo ni serikali iliingilia ndo maana zikapanda.
Zamani ilikuwa kila mtu anaweza la kwake, kwa sasa wamebanwa kama wauza mafuta
 
Habari za chini ya kapeti ni kwamba .....sababu ni mbili moja
1)kutafuta pesa ya kulipa mishahara mipya
2)kufunga watu midomo na masikio ya kwenye mitandao ili wasijue kinacho endelea maana mama hakubaliki hata chembe na raia wema yeye anakubalika na mafisadi tu
Hili ni kapeti la nyumba ipi mkuu?!
 
Wewe pandisha tu bei, tufidie hasara, watu tunawajua watapiga kelelee wee mwisho watazizoea tu bei mpya, na maisha yataendelea.

We amka embu uwapeleke wageni kituo cha mabasi,
aah.! jaman mngeniacha kidogo nilikua kwenye kikao. Kikao gani? Haa.! Kumbe nilikua naota,? Wamejiandaa tayar,..?!
 
Jana, nimenunua 640 MB kwa sh. 1000 lakini kuamka asubuhi 350 MB Ni kwa hiyo 1000. Kwa hiyo gharama imepanda mara mbili ndani masaa machache. Yote haya Ni kwa sababu upinzani wa Rais upo mtandaoni.

Hili balaa lilianza Baada ya huyu Rais kuingia madaraki. Kutokana na kusemwa sana akaanza kupandisha virushi.

Enzi za Magufuli kwa sh. 500 unapata 1GB - 500 mb , na alisisitiza sana taasi za serikali kuhamia mtandaoni.
Hii ilichangia ongezeko la internet users.

Madhara ya kupunguza watumiaji wa intaneti Ni makubwa :-

Kuwa na lundo la wasomi wasioendana na kasi ya duniani (wasomi wa vitabu).
Uhaba wa ma-programmer
Mifumo itakuwa ni analog
Hivi Leo Kuna watu ni matajiri kutokana tu na kucheza game online, (Ninja).
TUNAISOMA NAMBA CCM MBELE KWA MBELE
 
Back
Top Bottom