mtakatifu wa 2
Member
- Apr 15, 2022
- 22
- 45
Habari wanaJF,
Kwa wale tunao amini katika Mungu, kila uvumbuzi wa kiteknolojia unaofanywa na binadamu basi ni Mungu mwenyewe ameruhusu ukafanyike ili kutimiza mahitaji na matakwa ya binadamu katika ulimwengu huu.
Uvumbuzi wa internet(mtandao) uliofanywa na mwanadamu, Mungu ameruhusu ili uweze kumsaidia mwanadamu katika nyanja mbalimbali za maisha.
Kama vingine vyote vilivyofanyika kwenye ulimwengu huu Mungu amempa nafasi ya uchaguzi mwanadamu kati ya mema au mabaya, vivo hivyo hata internet mwanadamu ana nafasi ya kuchagua jinsi atakavyoitumia kwenye maisha yake aidha kwa kujenga ama kubomoa.
Moja kwa moja kwenye mada tajwa apo juu. Je, kwanini internet ni zawadi ya thamani?
Hizi ni baadhi ya faida utakazopata endapo utatumia internet kwa mlengo wa kujenga
1. Kujifunza ujuzi mpya.
Dunia ya sasa sio lazima kutumia gharama kubwa kumtafuta mbobevu wa ujuzi fulani ili akufundishe ujuzi huo, unaweza tumia kifaa chako chenye access ya internet kujifunza ujuzi huo bila gharama yeyote, kinachohitajika ni bando lako tu.kwa mfano mimi binafsi nimejifunza digital skills nyingi bila gharama yeyote. Hata humu JF unaweza kujifunza ujuzi kupitia nyuzi zinazotolewa na watu mbalimbali.
Baadhi ya skills nilizojifunza kupitia internet ni kama;
2. Kuuza/kununua ujuzi (freelancing)
internet imerahisisha sasa unaweza kuuza ujuzi wako bila wewe kusafiri kumfuata mteja ama mteja kusafiri kukufuata wewe,hii kitaalamu inaitwa work remotely. kama unaskills zifuatazo basi unaweza kuuza mtandaoni;
Na nyingine nyingi izo ni baadhi tu. application unazoweza kutumia kuuza ujuzi wako ni kama; Upwork ,workana na fiverr na linkedin, zote izi zinapatikana playstore ama apple Appstore.
Muhimu unapofungua account uko andika biography(wasifu) vizuri kumsaidia client kujua huduma unayoweza ku-offer kwake.
Mimi binafsi natumia upwork na fiverr kuuza ujuzi wangu nilioutaja awali.
3. Kufahamiana na watu wapya(connection)
Internet imewaunganisha watu pamoja kotoka kila kona ya dunia kupitia social media kama Instagram, Whatsapp, Telegram, Facebook,JF, Twitter,Dating sites kama Tinder,Tagged kote huko utakutana na watu ambao mnaweza saidiana katika moja na mbili.
4.Biashara
Kama wewe ni mfanyabiashara unaweza kuwafikia wanunuzi kupitia simu yako tu kwa kupost biashara yako mtandaoni muhimu weka mawasiliano yako na location biashara yako inapopatikana.
Kwa wanunuzi: Internet imerahisisha maisha sasa unaweza kununua bidhaa kutoka sehemu yoyote dunia bila wewe kasafiri kuifata bidhaa iyo,unacho hitaji ni access ya online market kupitia apps kama; Kikuu, Alibaba, Ebay, AliExpress, Amazon, Kupatana na nyingine nyingi. Mimi binafsi natumia apps hizi katika manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa reasonable prices kinachohitajika ni trust na uvumilivu tu.
5.Taarifa/habari
Internet imerahisisha utoaji na upokeaji wa taarifa mbalimbali punde tu zinapotokea kwasasa hautajiki kununua gazeti ama kusubiri taarifa ya habari redioni kwani taarifa zote unazipata kupitia social media.
Muhimu: Zingatia usitoe taarifa yoyote bila kuchunguza ama subiri vyombo husika vitoe taarifa hiyo.
Licha ya kuwa na faida mbalimbali internet pia inaweza kuwa silaha ya kuharibu maisha yako na kuharibu mtindo wa maisha uliozoea kuishi. Mfano mahusiano na wale wanaokuzunguka yanaweza kupungua endapo utatumia mda mwingi kwenye simu yako kuliko kujumuika nao kwenye maongezi ya hapa na pale. Biashara haramu na utapeli unafanywa kupitia internet ni vizuri ukaepukana nao.
Ahsante kwa muda uliotumia kusoma uzi huu ni matumaini yangu umebadilisha kitu katika mtizamo wa matumizi sahihi ya internet.

☞graphics designs
Sasa nina uwezo wa kutengeneza fliers,logo na posters kwa kitumia adobe photoshop na canva design.ujuzi huu nimeupata kupitia youtube na website zinazo toa online courses kama udems na edx, mahitaji muhimu ni curiosity ya kujifunza ,smartphone, pc na access ya internet basi. anza kwa kujiunga kwenye kozi za bure kupitia website tajwa apo juu baadae unaweza jiunga kwenye kozi za kulipia.
☞microsoft office application
Nimejifunza jinsi ya kutumia excel,word na powerpoint kupitia online courses zinazotolewa udems na edx kwasasa naweza sema nina intermediate skills kwenye hizi vitu, na zinanirahisishia kazi zangu mbalimbali sihitaji tena kupeleka kazi stationary hivyo imenipunguzia gharama.
2. Kuuza/kununua ujuzi (freelancing)
internet imerahisisha sasa unaweza kuuza ujuzi wako bila wewe kusafiri kumfuata mteja ama mteja kusafiri kukufuata wewe,hii kitaalamu inaitwa work remotely. kama unaskills zifuatazo basi unaweza kuuza mtandaoni;
~data entry
~language translation
~voice dubbing
~copywriting
~graphics design
~architectural design

Upvote
2