Tunaofanya kazi mahakamani, tunachoshwa na usanii huu. Huyu kijana katolewa, kamwacha Mwenzake kwa kipi hasa na huko alikopelekwa ni wapi, baadaye sisi tuanze kualaumiana. Binafsi naona kama DPP anadhalilika katika hili lakini ndo kunaonyesha nchi yetu inakoenda. Polisi wanatumia hadi mahakama kwa manufaa gani? kesi waliyofikisha mahakamani, wanaendaje kutoa mtu bila ruhusa toka kwa DPP? walipeleleza wakamaliza, wamepeleka kwa DPP, wamerudi tena kuja kuharibu wanavyotaka, na hakimu huyu aliyekataa siku ile, leo analazimisha mihuri itoke atumie kumtoa mahabusu kabla ya tarehe. Angalia