Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tumeshuhudia mara kadhaa mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, hususan ya Chadema, ikizuiwa na Polisi, kwa maelezo kuwa kwa taarifa zao "walizozinusa" mikutano hiyo italeta machafuko na hivyo kusababisha hatari ya maafa.
Hata hivyo, mtumishi wa Mungu, anayejiita Mtume Boniface Mwamposa, katika mkusanyiko mkubwa wa kidini, tukio la ukanyagaji wa mafuta huko mjini Moshi, limesababisha maafa ya wakazi wa huko, wasiopungua 20.
Kuondokewa na uhai wa angalau mtu moja, ni tukio baya kabisa. Sembuse raia wasiopungua 20?
Tunalifahamu Jeshi letu la Polisi lilivyo na utaalamu wa hsli ya juu wa "kunusa" matukio yatakayofuata, ikiwa chama cha siasa cha upinzani kinataka kufanya mikutano wake wa kisiasa katika maeneo mbalimbali.
Haraka haraka huzuia mikutano hiyo kwa madai ya kwamba Jeshi la Polisi limebaini kwa "kunusa" kuwa mikutano hiyo utakuwa siyo salama kwa wananchi kuhudhuria na hivyo kuipiga marufuku.
Ninachojiuliza hivi intelejensia ya Polisi ilienda "likizo" wakati wa kutokea maafa hayo ya mkusanyiko wa Boniface Mwamposa, hadi washindwe "kunusa" kuwa mkusanyiko huo wa kudini uteleta maafa makubwa sana?