Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Ni dhahiri, Msigwa alipojiunga CHADEMA, kama ilivyo kwa wengi waliokuja kukengeuka baadaye na kuamua kuwa mapandikizi, alikuwa ni mwanachama halisi aliyekuwa ameamua kuwa CHADEMA. Lakini wakati wa uongozi wa Magufuli, bila shaka, kwa hulka yake ya tamaa ya cheo, alishindwa kuhimili kuishi bila cheo na bila ya pesa. Akaamua kuwangukia CCM kwa namna ambayo aliamini haitamletea fedheha, akajisalimisha, na kwa kupitia yeye inaonekana kila taarifa za vikao vya ngazi za juu vya CHADEMA, Msigwa alizivujisha CCM. Na yeye akawa ndiye daraja la kuwaangamiza viongozi wenzake. Mawasiliano yake na hasimu wake wa sasa yanadhihirisha hilo.
Jambo la kujiuliza, je, intelijensia ya CHADEMA ni makini kiasi gani ili kuwatambua mapandikizi ya CCM ndani ya chama chao? Je, ndani ya CHADEMA, bado kuna akina Msigwa wangapi?
Ni dhahiri, kazi kubwa ambayo CCM ilimpa Msigwa ni kuipelekea CCM, mambo ya siri yanayojadiliwa na vikao vikuu vya CHADEMA. Hivyo baada ya kushindwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa kanda, nafasi ambayo ingemwezesha kuingia kwenye vikao vyote vya ngazi ya juu, hakuwa tena asset kwa CCM, na hivyo akalazimika kuomba kwenda kuhifadhiwa na wale ambao amekuwa akiwatumikia.