Kazi ya sheria hutegemea sana na idadi ya migogoro iliyopo katika jamii, angalia jamii yako kwa sasa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu kama vile haki ya kuishi, kutokuteswa, kutoa na kupokea habari, elimu, kazi, nk, kisha uone mwajiri hasa ni nani kama vile serikali au ngo, halafu angalia wimbi la ukiukwaji wa sheria za mali-akili, kama vile ukiukwaji wa hakimiliki ya watunzi mbalimbali,waimbaji na waigizaji, na je mwajiri wako katika secta hii anatarajiwa kuwa nani?? Hata hivyo kwa maoni yangu kuwa Sheria ya haki za binadamu ni kubwa kuliko sheria ya mali-akili kwakuwa kumiliki mali ni haki ya binadamu pia.