Interchange ya MWENGE na MOROCCO imepotelea wapi?

Interchange ya MWENGE na MOROCCO imepotelea wapi?

complex31

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
421
Reaction score
1,289
Habari,
Kwa watumiaji wa barabara ya Bagamoyo, Ali Hassan Mwinyi pamoja na viunga vyake vya Sam Nujoma kuna ujenzi unaendelea wa BRT phase ya 4.

Awamu iliyopita bwana Humphrey PolePole alisema kua kuna Interchange zitajengwa Makutano ya Bagamoyo na Sam Nujoma Road (Mwenge)
Makutano ya Ali Hassan Mwinyi na Kawawa Road (Morocco) na
Makutano ya Morogoro na Kawawa Road (Magomeni)
Kwa ujenzi unaoendelea hakuna dalili ya ujenzi wa Interchange yeyote katika makutano haya kwa kuangalia

1. Utanuzi na ujenzi wa Njia mbadala kupisha eneo la ujenzi wa Hizo Interchange
2. Mitambo ya kuchimba Mashimo ya nguzo ya hizo Interchange
3. Vituo vya BRT 4 kua karibu sana makutano ya hizi barabara
Tukumbuke BRT phase 1 kituo cha Ubungo Maziwa ilibidi kivunjwe na kusogezwa nyuma kupisha mradi wa Kijazi interchange.

Kwa Foleni za magari Mwenge na Morocco ni wakati sahihi kujenga hizi interchange kuepusha kupoteza muda barabarani na wananchi tutumie muda mwingi katika majukumu ya kujenga taifa na sio kwenye foleni za Daladala na magari.

Humphrey Polepole alisema pesa za kujenga Interchange hizi zipo tayari hivo basi nashauri mkandarasi wa sasa anaejenga BRT 4 aendeleze na hizi Interchange 3.


Unaweza andika Youtube “PolePole Interchange na ukapata Video akielezea mikakati ya hizo Interchange

View: https://youtu.be/f6ztH295mbc?si=7B4bO8T7_byPRQfI

Nawakilisha.
 

Attachments

  • IMG_8040.jpeg
    IMG_8040.jpeg
    745.7 KB · Views: 4
  • IMG_8039.png
    IMG_8039.png
    2.6 MB · Views: 6
Wajanja walisha pita nazo baada ya zile zama kumalizika na kitabu chake.
 
Back
Top Bottom