Interference & Non interference engines

KndNo1

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2021
Posts
627
Reaction score
2,049
Engine ya gari ina moving parts nyingi.. Kila moja ina kazi yake na mwendo wake..nyingine zinapanda zinashuka.. Nyingine zinazunguka kwa utaratibu maalumu.. Ili movements ziende kwa kufuata utaratibu/rhythm engine inabidi ifanyiwe timing.. Kuna timing belts na chains.

Ikitokea belt au chain kukatika, husababisha movements kwenda nje ya utaratibu.

Movements kwenda nje ya utaratibu kuna madhara.. Ukubwa wa madhara hutegemea engine yako ni Interference au ni Non Interference.

Interference..

Engines nyingi zipo kundi hili..
Hizi ni zile engines ambazo piston na valve zinashare njia..! Timing belt/chain ikikatika wakati unaendesha.. Piston na Valves zitakutana.. Italeta madhara makubwa sana kwenye engine.. Hasa ukiwa mwendo mkali..
Kupindisha valves..
Kuharibu pistons..
Kuharibu cylinder head..
Kubadilisha engine yote..!

Non-interference
Engine hizi ni zakizamani.
Hizi engine ni kinyume.. Piston na Valve haziwezi kukutana.. Hapa hata timing belt/chain ikatike hakuna madhara utapata zaidi ya kupaki gari pembeni na kubadilisha belt/chain.

Mifano yake
Toyota 7A kwenye Corolla
Suzuki G13B kwenye Samurai SJ413

Kutokana na mahitaji ya kupata power kubwa kwa engine ndogo.. Gari ziwezinatumia mafuta kidogo.. Emissions standards.. Imepelekea non interference engines kuwa nje ya soko.. Sababu hairuhisu valves kufunguka vizuri(poor airflow) na compression inakuwa ndogo kwenye engine.

Ni vizuri ukafahamu engine yako ipo kundi gani kama blood group yako.
 
Shida ya belt sio kitu utakagua kiurahisi kama coolant au engine oil..
Inabidi kucheza na kilometres..
Hapo ndio kazi ipo..
 
Sure mzee yani kuna vitu watu wanaona ni vidogo vidogo tu yani bongo mtu anajua kubadili oil na filter kamaliza na hata nyuzi kama hizi mtu anaona ni nyuzi za kuwaachia mafundi hata sijui tumerogwa na nani
 
Shida ya belt sio kitu utakagua kiurahisi kama coolant au engine oil..
Inabidi kucheza na kilometres..
Hapo ndio kazi ipo..
Sasa mkuu kama una diary ya kuweka kumbukumbu zako za muhimu kwanini na data za chombo unachotumia kila siku au kukuingizia kipato usiweke
 
Sasa mkuu kama una diary ya kuweka kumbukumbu zako za muhimu kwanini na data za chombo unachotumia kila siku au kukuingizia kipato usiweke
Unabadilisha baada ya 100,000kms.. Hapo miaka mingi itaipita..
Unasahau..
 
Unabadilisha baada ya 100,000kms.. Hapo miaka mingi itaipita..
Unasahau..
Ukisahau imekula kwako
Atleast mtu mwenye utaalamu kidogo akiiangalia tu ile ramani ya mipasuko anajua uhai wake ulivo otherwise imekula kwako

Hivi ya cheni najuaje kwamba inakaribia kuisha?
 
Ukisahau imekula kwako
Atleast mtu mwenye utaalamu kidogo akiiangalia tu ile ramani ya mipasuko anajua uhai wake ulivo otherwise imekula kwako

Hivi ya cheni najuaje kwamba inakaribia kuisha?
Kuna mlio wa kukwaruza kwaruza..!
 
Itafikia hatua gari utakuwa huazimishi kwa mtu ukihofia kupoteza data za kilometers
 
Kwa mfano 1NZ engine, inatakiwa ibadilishwe baada ya muda gani?
 
Ukisahau imekula kwako
Atleast mtu mwenye utaalamu kidogo akiiangalia tu ile ramani ya mipasuko anajua uhai wake ulivo otherwise imekula kwako

Hivi ya cheni najuaje kwamba inakaribia kuisha?
Wanaita rattle noise unaweza kusearch youtube hiyo noise inasikikaje.
 
kaka kuna gari nnayo noah sr40 inakata belt balaa inakua bado ni mpya kabisa. uzuri ni non interference so natembeaga na belt ya akiba tu ikikata naita fundi anabadilisha maisha yanasonga sijui shida ni nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…