Nimesikiliza vizuri interview ya Ommy...swala ni kwamba yeye alimchukulia Diamond kama mshikaji na akataka kila anachofanya Dee na yeye akijue au ashirikishwe, jambo ambalo Dee hakulitaka. Dee aliona kama Ommy anataka sana kujua kazi yake so akawa kama anamkwepa na hivi ashakua msanii mkubwa..kwahyo na kiburi kikaongezeka!
Ommy alichoongea kiko vizuri kabisa.. Riziki anatoa Mungu na yeye hashindani na Dee kabisaa...sema Dee anaonekana hapendi mtu yoyote ampite kwa chochote..na ana tamaa! Kila kizuri anataka kiwe chake..
Ommy kasema Kiba alikua mshikaji wake tangu mwanzo...na sio kwamba kisa haongei na Dee ndo amekua upande wa Kiba! Na kasema akikaaga na Kiba hizo habari za Dee hawaongei kabisaa...maana hata Kiba mwenyewe sio mzungumzaji kabisaa..
Anachoshangaa zaidi ni vile watu wanavyomuona Dee kama mungu mtu, kwamba yeye Ommy ndo ajishushe yaishee..badala waseme au wapange wakutanishwe wote sehemu ( kasema hata kwa AY) waongee yaishe! Yeye kasema hana shida..ana love ya kutosha kwa Dee na anaheshimu mchango wake!
Sehemu iliyonigusa...ni vile Ommy alivyosema..hadi siku Dee ananunua pikipiki yake ya kwanza ( kipindi huko Dee ndo anatoka kimziki) ..wanapakizana wote, wakifika sehemu za makorongo anashuka..then mshikaji chombo... Af leo huyo mtu anakwambia unapumuliwa!!! Ila Dee uswahili umemzidi..anatakiwa abadilike!! Yote mapito tu...walikuwepo akina R.Kelly enzi hizooo...leo kimyaaaa, haya maisha tu!