Ngoja nikueleweshe kwa manufaa ya wengi;
Tv nyingi zinazouzwa zikija mpaka kwa muuzaji hazina waya wa hdmi, hazina tv guard, hazina waya wa kuconnect na subwoofer, na nyingi inch 43 kushuka chini hazina bluetooth
Muuzaji anaweza kukupa hivyo vitu bure lakin kiuhalisia sio bure bali ame-jumuisha kwenye bei aliyokuuzia tv ndo maana muuzaji akikuuzia bei ya chini sana hawez kupa hata kimoja wapo, ila kama akikuuzia bei ya juu anaweza kukupa hivyo vitu kama bonus lakin-kiuhalisia ni wewe umevinunua indirect kupitia ile hela yako ya tv
Mfano kwa tv inch 43 kushuka chini hazina bluetooth kwa hiyo ukitaka kutumia bluetooth inabidi ununue bluetooth device kamwe hii sio sehemu ya warranty
Mfano ukitaka waya wa hdmi wenye ubora wa juu kabisa kama hdmi 30 ni elfu 40 na kuendelea, ukienda mwenge hadi elfu 60 wanakuuzia na huu hdmi 30 ni ngumu sana muuzaji kukupa kama bonus inabid ununue kama mteja, sababu hata ule unaopewa bure ni hdmi 1.5 au hdmi 5 na huwa hazina quality zina ubora wa chini sana, na kamwe waya wa hdmi sio sehemu ya warranty