Ipandwe miti pembeni mwa mto Mpiji

Ipandwe miti pembeni mwa mto Mpiji

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
3,443
Reaction score
4,006
Wana jukwaa JF na wizara husika ya mazingira
Napendekeza ipandwe miti pembezoni mwa mto Mpiji kuanzia daraja linalotengganisha Kibaha na Ubungo hadi Mbweni baharini katika pande zote zinazotenganisha Kinondoni na Mapinga, Bagamoyo ili kutunza mazingira ambayo yanaharibiwa kwa kasi kutokana na shughuli za kibinadamu pampoja na majenzi ya makazi
 
Unataka tozo liongezeke ww..kaa kimya hivo hivo
Wajasiriamali wanaotesha miti pembeni mwa mto na kuuza kwa watu wanaoenda kupanda maeneo mengine huku pembeni mwa mto miti yote imekatwa huoni huo ni uharibifu wa mazingira na kuhatarisha afya za watu lakini pia kusababisha mabadiliko ya tabia nchi ambapo madhara yake ni mtambuka? Zamani mto huo ulikuwa na maji yanatiririka mwaka mzima na kama maji yakipungua unyevunyevu uliendelea hadi msimu mwingine wa mvua. Mto huo unatokea Kisarawe na ndio tegemeo kubwa kufanya pori la akiba la Mabwepande kuwa endelevu vinginevyo kuna siku msitu huo utaingiliwa kwa nguvu na wananchi ili kupata maeneo ya kujenga.
 
Mto Mpiji wenye chanzo chake kutoka wilaya ya Kisarawe kupitia, Makurunge, Kiluvya, Kibaha, wilaya ubungo kupitia Mpiji magoe, Mabwepande, Bunju na Mbweni serikali inaombwa kwa mara nyingine kwa wema tu mto huo upandwe miti na shughuli za kibinadamu ziratibiwe na kudhibitiwa zisiendelee kusababisha madhara ya mmomonyoko wa udongo.

Ipandwe mti rafiki kwa uhifadhi unyenyevu kwenye udongo na mazingira kwa ujumla
 
Back
Top Bottom