Ipe neno picha ya leo

Hii picha kama siyo shuleni lakini ni mazingira fulani ya karibu na shuleni...

Ukichunguza vizuri inahuzunisha sana lakini inachekesha pia

Dogo anadondosha chozi haamini kilichompata halafu akiangalia mbele yake kuna bonge la shoka (anawaza sijui ni kwajili ya kukata mti au shingo)

Wenzake nao wamesitisha hata kwenda nyumbani/shuleni wanashuhudia mwenzao anavyohangaika na kulia

Kinachochekesha ni hilo shoka na usimamaji wa hao watoto pamoja na mwonekano wao kama wanafunzi

Yaani madogo wameduwaa mpaka wanakanyagana wengine bila hata kugundua na wamepauka balaa halafu kuna anayeonekana kabisa hapo kuwa yeye ndiye kamsababishia mwenzake
 
Wakafanyie tohara hapo hapo bila ganzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…