Ipi Adhabu sahihi kipa anapodakia nje ya 18

the muter

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2012
Posts
1,347
Reaction score
1,828
Wataalam naomba mnisaidie hili maana kuna mechi flan ilikua ya Yanga kipa alidakia nje akapewa direct red card, Jana simba na mwadui kipa alidakia nje akapewa yellow. Naomba kujua ipi ni sahihi au mazingira gan yanatofautisha red na yellow kwa kosa hilo?
 
Kadi nyekundu ilikuwa mechi ya Yanga na Njombe Mji. Kadi nyekundu ilitolewa kwa sababu ule mpira aliodaka kipa ulikuwa unakwenda ndani ya goli moja kwa moja na golikipa alifanya makusudi kabisa kudaka huku akiwa nje ya 18.

Mechi ya Simba na Mwadui golikipa alidakia ndani au tuseme kwenye edge, lkn akajikuta anatoka nao nje ya 18, lakini kubwa kuliko hakua amezuia mpira kuingia golini, alkuwa anaondoa hatari. Maamuzi yote waliyofanya marefarii hawa ni sahihi
 
Umefafanuwa vzr sana mkuu hongera kwa hilo.
 
pia ufafanuzi, refa anaruhusiwa kuudaka mpira na kupuliza kipenga cha mwisho?? kawaida tumezoea refa anapuliza kipenga cha kuashiria mwisho wa pambano kisha anaufuata mpira anaondoka nao, Ref: Game ya Simba vs Mwadui jana.
 


1. Kudaka makusudi ni Red straight.
2. Kudaka bahati mbaya ni Yellow
3. Kudaka bahati mbaya kwelikweli hiyo hakuna kadi la faulo ipo palepale..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…