Ipi bora; Kahawa au Energy drink?

Ipi bora; Kahawa au Energy drink?

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
- KAHAWA au ENERGY DRINKS (za viwandani) ipi bora?.

* KAHAWA: kinywaji cha asili chenye sifa ya kuongeza nguvu ya ziada kinachotokana na mimea.


* ENERGY DRINKS: Vinywaji hivi vya kuongeza nguvu ya ziada kutoka viwandani.
~Vinywaji hivi vimeibuka kuwa maarufu sana hasa kwa vijana ambapo vimeonekana kama mkombozi wao hasa kwa urahisi wa upatikanaji.

Ni nini kinacho patikana katika vinywaji hivi viwili ili kuwa na sifa ya kumpa mtumiaji nguvu ya ziada pale anapohitaji?

Hebu tufanye mlinganyisho wa pande zote na tuonekiafya pia ikoje?

Hivi ndivyo vitu muhimu vinavyofanya vinywaji hivi viitwe (kinywaji nguvu).

1) CAFFEINE:
Chupa ndogo ya energy drink (300 ml) na kikombe cha kawaida (≤ 300 ml), vyote vibeba kiwango sawa cha caffeine.

Hata hivyo, caffeine inayopatikana kwenye kawaha asili hunyonywa taratibu na mwili tofauti na ilivyo kwa energy drinks za viwandani.

Kivipi; caffeine inayopatikana kwenye vinywaji vya viwandani vimebuniwa ili kunyonywa kwa haraka na kufanya kazi haraka zaidi.

2) VIUNGO VYA ZIADA(additives):
Energy drinks zimebeba viungo vingine vya ziada ndani yake kama; Taurine ( amino sulfonic acid ), ginseng, preservatives, radha, rangi na vinginevyo vingi (kulingana na pendekezo la kiwanda).

Kawaha haina viungo kabisa au hutiliwa kidogo sana kama (preservatives) ili ikae kwa muda fulani bila kuharibika kwa haraka.

3) VIRUTUBISHO
Kahawa ina vitamin B2, B5, B12, potassium, niacin, sodium na magnesium.

Energy drinks pia ina vitamins B', niacin, lakini pia Taurine na ginseng, sukari na vitu vingine ambavyo havihitajiki sana na mwili.

4) SUKARI
Energy drinks zina kiwango kikubwa cha sukari kuliko kahawa.

Hata hivyo, unaweza kuongeza kiwango cha utamu katika kahawa kulingana na apendavyo mtumiaji.

FAIDA KIAFYA:

Kahawa ni bora na salama zaidi kiafya kulingana tafiti zilizokusanywa kwa karne nyingi.

Energy drinks hazina shida lakini zina maonyo mengi kudhibiti utumiaji holela, kutokana na uwezo wake wa juu wa kuweza kumsababishia mtumiaji Matatizo ya kiafya hasa ya moyo ikitumiwa kupita kiwango.
 
Bora kahawa tu energy drinks ni dangerous ila zinaa ndio inasababisha energy drinks zipendwe zaidi maana hapa dukani kwangu kuna madada wanakuja kununua pamoja na panadol kila siku usiku yaani wanapeana tu zamu huyu anakuja leo kesho anakuja mwingine yule wa jana anapumzika
 
Zote SI nzur..kuna siku nlifululiza ka siku tatu nakunywa kahawa...nikaanza kuskia kama joints zinaniuma...kwenda kupima wakanambia uric acid imepanda sanaa...tangu hyo siku situmii tena
 
Coffee, The old school Energy drink

IMG_20240615_075014_440.jpg
 
Back
Top Bottom