Ipi bora utashi wako au sheria

Ipi bora utashi wako au sheria

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
Sisi binadamu tumepewa uwezo wa kutafakari na kutambua mabaya na mazuri.
Kanuni rahisi ya kujua kama jambo ni baya au zuri ni kujiuliza kama ingekuwa linakutokea kwako ungejisikia vipi, au kama ni wewe ndiye ungekuwa huyo mtu mwingine ungejisikia vipi.
Ni kanuni moja rahisi sana, lakini pia ni ngumu kwa kuwa:-
1. Huwa wengi hawawazi kujiweka nafasi ya mtu mwingine. Yaani kwa haraka kufikiria kama ni wewe huyo mtu mwingine unayemtendea jambo ingekuwaje?
2. Haujajingea uwezo wa kufikiri mambo wewe mwenyewe na kujiamini katika maamuzi yako. Mengi unayoamini na kuamua ni kwa kufuata mtazamo wa kanuni ambazo tayari umeshawekewa na watu wengine. Unapima zaidi uhalali wa jambo kwa kuangalia kanuni au sheria zilizowekwa kuliko kuamini katika usahihi au jambo kutokuwa sahihi kwa kujilinganisha na wewe mwenyewe kama ungekuwa ndio mhusika wa kutendewa jambo hilo.
3. Wakati mwingine unakuwa mtu wa ajabu kweli kweli eti unaogopa kutenda kwa usahihi hata kama unajua ulitakiwa kutenda kwa usahihi, kwakuwa tuu unadhani hautopata malipo sawa sawa toka kwa mtu husika (Yaani mtu husika hatokuwa mwema kwako utakapohitaji msaada wake).
Hivyo unajikuta pamoja na kujua usahihi, bado unaamua kwa makusudi kufanya isivyo sahihi. Na zaidi sana unafanya hivyo kwakufuata tuu mkumbo au maneno ya watu wengine, unaacha kusikiliza sauti yako toka moyoni inayokutaka utende kwa usahihi
.


 
...kuna kitu kizuri umetaka kukieleza, lakini nafikiri, haujawa wazi, umefungafunga sana, maana mwanzo umetaja Utashi na Sheria... sasa suala la mtu kufanya maamuzi yake binafsi sheria inahusika vipi, mfano kuoa, kununua gari n.k.
....mi nafikiri ungezungumza wazi tu kama kuna chombo ulitaka kukizungumzia tungeweza changia vizuri......besides...hicho unachokiwaza ni kwamba sheria na utashi vyote vinatumiaka na ndio maana watu wanasoma Jurisprudence
 
Back
Top Bottom