Ipi hatima ya CHADEMA baada ya minyukano inayoendelea?

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Chadema kinashuhudia minyukano ya wazi na hatarishi mno tokea kianzishwe. Unaweza kusema pasi na shaka, sasa kuna Chadema mbili. Mosi, Chadema ya Mbowe. Na pili, Chadema ya Lisu.

Chadema hizo mbili zinanyukana isivyo kawaida!

Je, ni rasmi anguko la Chadema linaenda kutukia?

Ipi hatima ya Chadema baada ya Uchaguzi wa Viongozi wake Wakuu mnamo baadae Mwezi huu wa kwanza?
 
Tutegemee CDM imara zaidi kuliko ile ya jana. Hakuna jingine.
 
Tatizo ni kuropoka kwa Lisu
 
Tutegemee Chama dola kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu mwaka huu
kwasababu upinzani umebakia ni hopeless
 
Atokee jina geni mwenye upeo wa kugombea uenyekiti huyo atakiokoa chama
 
Ukitaka maswali Yako hayo yapate majibu ni lazima kwanza ujue yafuatayo:
1. Nini kilimtoa Zito kabwe, Dr. Slaa na wengine wengi mashuhuri CHADEMA?
Ndipo utajua hii vita haijaanza Jana ni muendelezo na aliekiamsha anastahili pongezi japo ndio wao kwao wanamuona adui, mropokaji etc..

Vita ya kiuchumi ni mbaya sana, daima tuuchukie umaskini.
 
Baada ya uchaguzi hakutakuwa na minyukano.
This is one of the principles of thermodynamics.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…