Ipi ni hatma ya lugha yetu pendwa kiswahili katika awamu ya sita?

Ipi ni hatma ya lugha yetu pendwa kiswahili katika awamu ya sita?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Habari wana JF,

Nimesikiliza hotuba ya muheshimiwa Raisi kwa uzuri kabisa nikamwelewa, lakini lugha hii yetu pendwa (kiswahili) hajazungumzwa mahala popote.

Hapo awali kiswahili kilitiliwa mkazo kwa sababu zinazojulikana na utawala uliopita. Lugha ya kiingereza ilionekana ni anasa au kielelezo cha kuukubali na kuukiri ubeberu. Watawala walijinasibu kuongea kiswahili kwenye halaiki zenye watu wasiokijua. Mipango iliwekwa ili hukumu za mahakama zitolewe kwa lugha yetu, pia na mitaala yetu ya shule iwe ya kiswahili.

Ukimya huu, kuhusu lugha yetu unaashiria nini? Embu wadodosi wa mambo mtujuze
 
Kiswahili kilizikwa rasmi palee kwa M7 kwenye hotuba ya Bi Mkubwa.


Jina: Kiswahili

Wadhifa: Lugha ya Taifa

Muda wa Kushamiri: Desemba 1961 - 1984 & 1985 - 1995 & 2015- 2021

Umauti: 17.03.2021 palee Mzena Hospital

Kuzikwa: Uganda kwa M7
 
Back
Top Bottom