Ipi ni sentesi sahihi?

Ipi ni sentesi sahihi?

Joined
Feb 2, 2014
Posts
31
Reaction score
2
Hivi ipi ni sentensi sahihi kati ya:
'Naomba unipigie nyimbo ya Madee na Naomba nipigie wimbo wa Madee? Wafunzi wananikera sana. Msaada wenu tafadhali.
 
ndo mfano unaotumika darasan kwa wanafunzi? Ndio maana ufaulu unashuka,BRN
 
Hivi ipi ni sentensi sahihi kati ya:
'Naomba unipigie nyimbo ya Madee na Naomba nipigie wimbo wa Madee? Wafunzi wananikera sana. Msaada wenu tafadhali.

Mkuu mimi kama mswahili naona kiswahili fasaha hapo itakuwa 'Naomba unipigie nyimbo ya Madee' neno Unipigie inamaanisha unamuomba mtu

lakini 'Naomba nipigie wimbo wa Madee' sio sahihi kama unaomba,kwani neno nipigie ni neno la kuamrisha sio la kuomba
 
Wale wale Mulugo generation wimbo ni umoja na nyimbo ni wingi dah ulivyoandika insha sasa kama una point vile teh teh
 
zote mbili sio sahihi, sahihi ni:- naomba unisikilizishie wimbo wa madee, unasikia baridi au unahisi baridi? dawa ya mswaki au ya meno?, nimemkuta hayupo?,Think twice.
 
Wimbo(umoja)
Nyimbo(wingi)

1.Naomba Nipigie Wimbo Wa Madee

2.Naomba Nipigi Nyimbo Za Madee
 
1.Nipigie:- ,piga pigilia pigika pigwa pigania piganiwa kipiganishi[kipigio]
2.sikilizisha:-sikiliza,sikia sikiliza, sikilizishia, sikilizishiwa kisikilizishio[sikio]
 
Wale wale Mulugo generation wimbo ni umoja na nyimbo ni wingi dah ulivyoandika insha sasa kama una point vile teh teh

Mkuu hapo sikuangalia wingi na uhaba isipokuwa nimeangalia sentensi nzima na ndio maana nimeweka bold hayo maneno niliyatoa kasoro,sasa kasoro kuhusu wimbo na nyimbo sijui zimetoka wapi 😉

kama unataka kujua wingi wa "nyimbo" ni "majimbo" kama mnavyosema wingi wa ¨'gari' ni 'magari' 🙂
 
Back
Top Bottom