Ipi ni Tafsiri Sahihii?

Ipi ni Tafsiri Sahihii?

8691jakigili

Senior Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
179
Reaction score
67
Is it possible that every denomination is right?

Je, inawezekana kwamba kila madhehebu ni sahihi?

Au, Je, kuna ukweli kwamba madhehebu yote ni sahihi? Ni sahihi kusema madhehebu haya au hii ikiwa unazungumzia kikundi kimoja?

Pia, naomba msaada wa neno la Kiingereza "parable" kwa Kiswahili.

LUGHA yA KISWAHILI NI URITHI WETU, TUJIVUNIE!
 
Is it possible that every denomination is right? = Je, inawezekana kwamba kila madhehebu ni sahihi?

parable = mithali; mfano
 
Ukiweka kibainishi cha idadi 'kila', nomino inyosemwa lazima iwe katika umoja. Kwa hiyo sentensi sahihi inaweza kuwa 'Je, Inawezekana kila dhehebu ni sahihi?'

NB: Hakuna namna moja ya kutafsiri kimuundo, la msingi ni maana inayolengwa na ukubalifu wa maneno.
 
Je, tofauti kati ya sentensi, 'Je, Inawezekana kila dhehebu ni sahihi?' na 'Je, inawezekana kwamba kila madhehebu ni sahihi?' ni nini?
 
Tofauti ipo katika matumizi ya kiambishi cha uwingi katika sentensi ya pili 'ma-dhehebu' ambayo inaifanya isiwe sahihi kwani inatanguliwa na kibainishi cha idadi 'kila'. Unapotanguliza kibainishi hiki cha idadi, nomino inayobainishwa lazima iwe katika umbo la umoja. Mf. 'Kila mmoja', 'kila mtu' 'kila mwanaume' na kadhalika....
 
Asante! Kumbe, nilikosa! Nilisoma kwa haraka mno basi sikutambua uliandika 'dhehebu' badala ya 'madhehebu'!

Hata hivyo, nilitafuta neno hili kwenye kamusi mbalimbali, lakini katika TUKI Kamusi neno 'dhehebu' halipo. Kamusi zote zinaonyesha kwamba neno 'madhehebu' linatumiwa kama 'singular' na 'plural'. Kamusi mbili zilitaja tu kwamba 'dhehebu' ni 'derived word' (lakini kwa ujumla halitumiwi), lakini 'madhehebu' linatumiwa kwa 'moja' na kwa 'uwingi'. Pia, ninapokuwepo Tanzania watu wanalitumia 'madhehebu' kwa 'singular' na kwa 'plural'. Kwa hiyo, sentensi, ''Je, inawezekana kila madhehebu ni sahihi?' ni sawa. Tafuta kwenye kamusi. Je, unaweza kuona tofauti?
 
Hilo ni kati ya maneno machache ambayo yapo katika wingi tu, lakini kutokana na matumizi kumekuwa na umbo la umoja pia... Mengine ni 'mashtaka' na 'majukumu'. Kamusi ya TUKI toleo la 2013 limeweka neno hili katika umoja, lakini bado msisitizo ukiwa katika umbo la wingi. Tofauti uliyoitaja nimeiona na nimeitambua....
Asante! Kumbe, nilikosa! Nilisoma kwa haraka mno basi sikutambua uliandika 'dhehebu' badala ya 'madhehebu'!

Hata hivyo, nilitafuta neno hili kwenye kamusi mbalimbali, lakini katika TUKI Kamusi neno 'dhehebu' halipo. Kamusi zote zinaonyesha kwamba neno 'madhehebu' linatumiwa kama 'singular' na 'plural'. Kamusi mbili zilitaja tu kwamba 'dhehebu' ni 'derived word' (lakini kwa ujumla halitumiwi), lakini 'madhehebu' linatumiwa kwa 'moja' na kwa 'uwingi'. Pia, ninapokuwepo Tanzania watu wanalitumia 'madhehebu' kwa 'singular' na kwa 'plural'. Kwa hiyo, sentensi, ''Je, inawezekana kila madhehebu ni sahihi?' ni sawa. Tafuta kwenye kamusi. Je, unaweza kuona tofauti?
 
Wadau nawashukuru sana kwa mchango wenu wa kuidadavua lugha ya Kiswahili. Nimependa michango yenu iliyosheheni maarifa. Naomba radhi kwa kuchelewa kuwapongeza kwa michango yenu!
 
Back
Top Bottom