8691jakigili
Senior Member
- Mar 30, 2012
- 179
- 67
Is it possible that every denomination is right? = Je, inawezekana kwamba kila madhehebu ni sahihi?
parable = mithali; mfano
Ukiweka kibainishi cha idadi 'kila', nomino inyosemwa lazima iwe katika umoja. Kwa hiyo sentensi sahihi inaweza kuwa 'Je, Inawezekana kila dhehebu ni sahihi?'
NB: Hakuna namna moja ya kutafsiri kimuundo, la msingi ni maana inayolengwa na ukubalifu wa maneno.
Je, tofauti kati ya sentensi, 'Je, Inawezekana kila dhehebu ni sahihi?' na 'Je, inawezekana kwamba kila madhehebu ni sahihi?' ni nini?
Tofauti ipo katika matumizi ya kiambishi cha uwingi katika sentensi ya pili 'ma-dhehebu' ambayo inaifanya isiwe sahihi kwani inatanguliwa na kibainishi cha idadi 'kila'. Unapotanguliza kibainishi hiki cha idadi, nomino inayobainishwa lazima iwe katika umbo la umoja. Mf. 'Kila mmoja', 'kila mtu' 'kila mwanaume' na kadhalika....
Asante! Kumbe, nilikosa! Nilisoma kwa haraka mno basi sikutambua uliandika 'dhehebu' badala ya 'madhehebu'!
Hata hivyo, nilitafuta neno hili kwenye kamusi mbalimbali, lakini katika TUKI Kamusi neno 'dhehebu' halipo. Kamusi zote zinaonyesha kwamba neno 'madhehebu' linatumiwa kama 'singular' na 'plural'. Kamusi mbili zilitaja tu kwamba 'dhehebu' ni 'derived word' (lakini kwa ujumla halitumiwi), lakini 'madhehebu' linatumiwa kwa 'moja' na kwa 'uwingi'. Pia, ninapokuwepo Tanzania watu wanalitumia 'madhehebu' kwa 'singular' na kwa 'plural'. Kwa hiyo, sentensi, ''Je, inawezekana kila madhehebu ni sahihi?' ni sawa. Tafuta kwenye kamusi. Je, unaweza kuona tofauti?