Ipi nichukue kati ya IST na Golf 4 GTI

zhang laoshi

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
434
Reaction score
581
Polen na mihangaiko ya maisha, katika kujipanga kimaisha kuwa na gari or kuwa na ndoto ya kumiliki gari ni muhimu coz inaturahishia mishe zetu mjini, nime make tuela kangu, sasa sijui ipi nichukue kati ya gari aina ya IST na Volkswagen Golf 4 GTI, please msaada kwa anayezijua zaidi kifaida na kihasara, ili nimake decision soon. Ili nami nijue bei ya mafuta sheli.


IST


Golf 4 GTI
 
Kwakuwa ni gari yako ya kwanza chukua ist mkuu.

Lakini acha kufananisha gari na usafiri mkuu.

Huwezi fananisha gofu vw na ist mkuu dharau hizooo
 
VW Vs IST= sumsang Vs iPhone. Irrelevant comparison
 
To me, nikiangalia spares availability, IST MKUU...
 
Kwa ushauri wangu usichukue VW Golf, Chukua VW Polo 2007 Model au juu; Utaifurahia na kufurahia maisha ya kuingia Petrol Station.
Angalizo, spares za VW bei ni juu kidogo so unaweza tishika, ila spares zake ni original so zinakaa muda mrefu. Kila la heri kwenye uchaguzi.
 

Pamoja mkuu
 
Mkuu VW golf kama unaanza kumiliki gari itakutesa, pia kama huna knowledge na ufundi kwa mafundi wetu hawa watakutia hasara labda kama utakuwa unaipeleka kwenye modern garage lakini kwa hawa mafundi wetu wa uswazi itakucost, gharama ya spea ni kubwa na availability ya spea ni complicated kwa hapa bongo,

Ila kama unapenda maspeed kama mimi Golf ni nzuri na inakimbia lakini kwa barabara zetu pia itakulimit, ziko sensitive kwa mafuta pia, BP,TOTAL ndio uweke mafuta lakini hizi petrol station za kibongo aisee utaua fuel pump kila siku na fuel pump ni zaidi ya 300000/ wakati za kijapani ni 80000/

Ist ni nzuru kwa mazingira yetu, spea parts zinapatikana na ni rahisi pia, pia ni rafiki kwa mafundi wetu...
 
Toa neno GTi fananisha VW Golf ya kawaida tu 1.6i hivi kwasababu GTi ni perfomance car na IST ni gari ya kawaida tu. Katika gari rahisi kuhudumia kutoka Ulaya ni VW Golf hapa Tz nyingi ni mk4. Kama unaona kuhudumia vw golf mk4 ni ghali usijaribu gari ingine yoyote ya Ulaya.

Napenda kukujulisha wewe na wengineo vw golf mk4 spare parts ziko kibao kama toyota, hadi zilizokatwa zipo.
VW Golf 4


VW Golf 5
 
Ni kweli kabisa, ila nadhani ni lazima pia hiyo availability ya spare ya IST ufahamu na UBORA wake, nenda pale KISANGANI ulizia fuel pump original ya IST; nikimaanisha kama hiyo iliyokuja na Gari toka ulipoiagizia; bei zinafanana kabisa.

Mfano mrahisi nanunua oil filter kwa 30,000/=, naweka oil ya 75,000/= ila natembea km 9,000 bila wasiwasi. Mafundi ni kweli pasua kichwa ila kwa sasa kuna mafundi wazuri tuu wanatengeneza hizo gari.
 
Volks Bw Golf4 Spea zake ni very expensive na hupatikana kwa shida na inakula mafuta nunua TOYOTA IST ni na fuu saana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…