Ipi njia bora ya kujifungua kati ya operation na kawaida?

Siande

Senior Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
194
Reaction score
58
Wadau habari zenu,

Naombeni wenye uzoefu ntujuze kati ya kufanyiwa operation na kujifungua kawaida kwa mtu ambaye hana matatizo yanayompelekea kufanyiwa operation.

hii ni kwa sababu limetokea wimbi la wanawake ambao wako tayari kumuonga dr aandike sababu za uwongo ili afanyiwe operation kuliko kysubiria kuumwa uchungu na hawataki kusikua hiyo kitu uchungu.

Mfano ni rafiki yangu alijifungua kwa operation mi nkajua kulikuwa na complication mara akawa anasema mie nilimwomba dr aandike sababu za uwongo kwani hayo mambo ya uchungu na kupush sitaki kuyasikia.

Hicho ni kisa ambacho nina ushahidi nacho sasa ebu wazoefu waje kutujuza maana wapo waliozaa kawaida na kwa operation.
 
Huyo rafikio ni uoga tu uliompelekea aombe upasuaji na kukwepa adhabu na makusudi ya Mungu kwa mwanamke. Njia nzuri ya kujifungua ni ya kawaida kama mtu hana tatizo
 
Njia nzuri ni ya kawaida mda mfupi unakua fresh. Hyo operation ni kilema cha maisha. Ukijifungua tumbo linabaki kuwa kubwa ka nini. Pia siku hizi wadada wengi hutoa ule mtandao pendwa sasa siku za kujifungua Ku push inakua shida so best option ni operation.
 
Elewa kwa makini Mungu alituumbia tujifungue kawaida. Kujifungua kawaida ni salama na ni nzuri zaidi hata mara mia zaidi ya operation.
Ukijifungua salama baada tu yakujifungua hutasikia maumivu tena unakuwa salama kabisaa unasaahau na maumivu

tumbo lako linarudi kuwa dogo la kawaida tofauti na operation ambayo ni vigumu kurudi tumbo kwenye saizi yake.
Operation ni kidonda cha maissha ile alama haitatika na pia ukipata baribi mshono huwa unauma
Wenzio tulojifunsua salama hapa hata tukimwambia mtu tumezaa anakataa maana mwili uko vilevile hakuna mabadiliko makubwa ya kimaumbile kama ukijifungua kawaida.
Ewe mwanamke muombe Mungu ujifungue kawaida.
 
kujifungua kwa njia ya kawaida ni vizuri zaidi cha msingi uhakikishe unajifungulia mahali salama kwa watu makini. Ukiacha wale wanaojifungua kwa njia ya kawaida na kuongezewa njia, wanaojifungua kwa operesheni hubaki na maumivu ya kidonda na kovu husumbua wakati wa baridi kama alivyokwisha sema mtu hapo juu. Kuhusu ukubwa wa tumbo hakuna tofauti kati ya aliyejifungua kwa operesheni au kawaida. Naongelea uzoefu. Ukubwa wa tumbo hutegemea maumbile binafsi ya mtu, vyakula anavyokula mtu baada ya kujifungua, kiwango cha kunyonyesha n.k. Ukinyonyesha na kula kwa mujibu wa taratibu za lishe bora tumbo lako litarudi vizuri tu taratibu. Unaweza pia kuanza mazoezi kidogo baada ya miezi mitatu.

Kwa kuwa unajua kutumia mtandao google faida na hasara za njia zote mbili na ukumbuke kulinganisha utakachokisoma huko na mazingira ya kibongo.
 

Sawa bibie Princess sayuni
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…