Ipi sababu ya NBAA kuchelewesha matokeo?

Ipi sababu ya NBAA kuchelewesha matokeo?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Bodi yetu pendwa ya wahasibu na wakaguzi huwa wana utaratibu wa kutoa matokeo mapema kabla ya Julai kwa mitihani ya May na kabla ya mwaka mpya kwa mitihani ya November.

Kwa hii mitihani tuliyoifanya November naona bado kimya tu na sio kawaida yao kuchelewesha results kwa kiasi hiki. Kuna tetesi ya kwamba ongezeko kubwa la fresh graduates wanaounga moja kwa moja CPA kumefanya zoezi la usahishaji kuwa taratibu na hvyo kuchangia kuchelewa kwa matokeo.

Any way kwa niaba ya watahiniwa wote tunawaomba N.B.A.A mfanye jitihada kuwahisha matokeo ili tujipange kurepeat masomo tuliyofeli au kujiandaa kufata magamba yetu ya CPA.
 
Posho za Wasahihishaji mitihani Labda nasema Labda ndio zimechelewa hivyo nao wamegoma kukabidhi Matokeo , nasema Labda sina uhakika
 
Profession bodies za Tanzania zimekaa kijanja janja sana, hazina consistency.

Ukiwa na uwezo ni kusoma profession za nje ya nchi tu.

Nchi haina dira wala uelekeo, hakuna jambo lenye uhakika Tanzania. Kila kitu ni magumashi tu.
 
Umeshatoa sababu kuwa ni fresh graduate ndiyo waliosababisha kuongezeka kwa kazi ya kusahihisha.so kumbe jibu unalo
 
Back
Top Bottom