Bodi yetu pendwa ya wahasibu na wakaguzi huwa wana utaratibu wa kutoa matokeo mapema kabla ya Julai kwa mitihani ya May na kabla ya mwaka mpya kwa mitihani ya November.
Kwa hii mitihani tuliyoifanya November naona bado kimya tu na sio kawaida yao kuchelewesha results kwa kiasi hiki. Kuna tetesi ya kwamba ongezeko kubwa la fresh graduates wanaounga moja kwa moja CPA kumefanya zoezi la usahishaji kuwa taratibu na hvyo kuchangia kuchelewa kwa matokeo.
Any way kwa niaba ya watahiniwa wote tunawaomba N.B.A.A mfanye jitihada kuwahisha matokeo ili tujipange kurepeat masomo tuliyofeli au kujiandaa kufata magamba yetu ya CPA.