Ipi sahihi baina ya "Vita ya" na "Vita vya"

Ipi sahihi baina ya "Vita ya" na "Vita vya"

chabuso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
6,380
Reaction score
5,884
Katika kusoma magazeti ya kiswahili nimeona waandishi wengi wanapozungumzia vita sentensi huwa mfano:"Vita ya pili ya dunia" badala ya "Vita vya pili vya dunia" sasa wanaForum hebu tufahamishane kidogo garama gani iko sahihi
 
ya pili ndio sahihi

Nakubaliana na wewe madameX sasa kwanini hawa waandishi wetu wa mageziti wanakuwa wanaandika "Vita ya " huo sio ndio upotoshwaji wa kiswahili,wakati sisi watanzania tunatakiwa tuwe vinara wa kukitangaza kiswahili sanifu
 
mara nyingi lugha hutumia upatanisho wa kisarufi kwa hiyo maneno yote yanatakiwa yawe katika upatanisho wa kisarufi katika kuzungumza au kuandika.
 
Lugha ya kiswahili ina ngeli tisa ambazo huonyesha namna upatanisho wa kisarufi. Wanatakiwa kujikita zaidi katika misingi ya lugha wanayofanyia kazi.
Mfano wa ngeli:ngeli ya kwanza YU-A-WA
 
Back
Top Bottom