Katika kusoma magazeti ya kiswahili nimeona waandishi wengi wanapozungumzia vita sentensi huwa mfano:"Vita ya pili ya dunia" badala ya "Vita vya pili vya dunia" sasa wanaForum hebu tufahamishane kidogo garama gani iko sahihi
Nakubaliana na wewe madameX sasa kwanini hawa waandishi wetu wa mageziti wanakuwa wanaandika "Vita ya " huo sio ndio upotoshwaji wa kiswahili,wakati sisi watanzania tunatakiwa tuwe vinara wa kukitangaza kiswahili sanifu
Lugha ya kiswahili ina ngeli tisa ambazo huonyesha namna upatanisho wa kisarufi. Wanatakiwa kujikita zaidi katika misingi ya lugha wanayofanyia kazi.
Mfano wa ngeli:ngeli ya kwanza YU-A-WA