Ipi sahihi njano au dhahabu katika bendera ya Taifa

Ipi sahihi njano au dhahabu katika bendera ya Taifa

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Mjadala kuhusu rangi za bendera ya Taifa la Tanzania ni mzito kuliko nilivyodhani. Nimepekua baadhi ya nyaraka za kimataifa na zenyewe zinakinzana. Bendera ya Tanzania ilizinduliwa rasmi Tarehe 30, Juni 1964, ikiwa na rangi nne zenye maana zake. Tulipokuwa shule ya msingi tuliimba shairi moja hivi;

Bendera ya Tanzania, Ndio ya kujivunia,
Ilianza kupepea, Mwaka sitini na moja,
Hapa tunashuhudia, tunavyojitegemea,
Muumba wetu Rabuka, Ijaze yako fanaka. [emoji23][emoji23][emoji23]

Siku ya tarehe Tisa, Saa sita kamili,
Mwezi wa kumi na mbili, yalikuwa mambo sasa,
Mlima Kilimanjaro, Bendera yetu kuwekwa,
Mwenge haukubakia, nao pia uliwekwa.

Sasa unafuata ubeti unaohusu rangi.

Rangi ya chanikiwiti, huonesha mbuga zetu,
"MANJANO" ndio madini, yaliyo chini mwetu.
Buluu huonesha, Maji ya nchini mwetu.
Nyeusi ni yetu sisi, waafrika asilia,
Muumba wetu Rabuka, Ijaze yako fanaka.

Sasa kuna mjadala wa rangi ya 'MANJANO'. Je ni MANJANO au dhahabu?
Tangazo la wizara ya mambo ya ndani (Mwezi Novemba 2018) linasisitiza kuwa ni makosa kutumia rangi ya "MANJANO", badala yake, bendera ya Taifa ina rangi ya DHAHABU. Wakati huo, bandera zote, kama sio 99% za taifa zinazopepea sasa hivi nchini, ikiwemo ya ikulu, na wizara ya mambo ya ndani yenyewe, zina rangi ya MANJANO.

Kipi ni sahihi? MANJANO au DHAHABU.
Tuanzie kwenye Historia.

Baada ya TANU kushinda viti vingi vya uwakilishi kuanzia mwaka 1957/58 hadi 1960/61, serikali ya kikoloni ilitoa ushauri kwa chama cha TANU, kuboresha rangi na alama za bendera ya chama ili kupata bendera ya Taifa, kama sehemu ya kujiandaa na uhuru. Ushauri huo uliongeza kwamba, bendera ya Taifa iwe na ishara ya utajiri wa nchi.
Bendera ya TANU ilikuwa na rangi mbili, kijani na nyeusi, zilizopangiwa kwa mistari mitatu iliyolala. Mistari ya juu na chini kijani, katikati nyeusi. (Picha 1)

Maboresho yaliyofanyika kutokana na ushauri huo ni kuongeza rangi ya 'DHAHABU' kwenye bendera ya TANU ili kupata bendera ya Tanganyika. 'Vistari' viwili vikaongezwa juu na chini ya utepe mweusi (picha 2).
Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 1964 ikaamuliwa bendera za mbili za nchi hizo mbili ziunganishwe na kupata bendera moja.

Ndipo tukapata hii bendera yetu nzuri ya leo (Picha 4), bendera nzuri sana. Rangi ya buluu iliongezeka kutoka bendera ya Zanzibar (Picha 3).
Sasa MANJANO yametoka wapi?
Ukimsoma mwanahistoria Whitney Smith kwenye kitabu cha kumbukumbu ya mambo na matukio cha Encyclopædia Britannica, pamoja na mwanahistoria Dorling Kindersley's kwneye "Complete Flags of the World " wanaeleza kuwa vistari viwili vinavyolala mshazari kutoka pembe ya juu kulia hadi pembe ya chini kushoto, ni rangi ya MANJANO.

Vyanzo vingine kama "The World Factbook" pamoja na Simon Clarke katika jarida la "Azania" Archaeological Research in Africa, vinadai vistari vile ni vya DHAHABU.
Nyaraka za TANU zinaonesha ni DHAHABU.

Kizungumkuti ni kwamba kinyaraka, inaonekana kama DHAHABU ndiyo rangi iliyokusudiwa, kwa sababu Nyaraka zinazotaja DHAHABU zina uhalisia zaidi. Lakini undishwa darasani na kujionea kila kona ya dunia bendera yetu ikiwa na rangi ya MANJANO.

Nini kilitokea, Tafsiri ya wengi iliyofanywa kwa macho tu, ikasambaa ulimwenguni kote?
Kushindwa kutangaza vema alama yetu muhimu ya Taifa? Au ni Mazingaombwe kama tulivyozoea?
What happened?

Nadhani huu ni mjadala wa kitaifa zaidi. Christopher Cyrilo hawezi kuwa na majibu ya mwisho. Tunahitaji mjadala zaidi.
Nawasilisha.
FB_IMG_1544939026588.jpeg
 
Inaonekana Dhahabu ndio rangi ya bendera ya taifa kisichoeleweka ni nani alaileta rangi ya njano kwenye fahamu zetu hata mitaala na vitabu vinavyotoka wizarani vikapitisha rangi ya njano ifundishwe.
 
May be we stick to yellow because we lost too much gold,,,,
 
Back
Top Bottom