Ipi siri ya "Google Search" Kuyapa kipaumbele kwenye mpangilio mambo ya kipuuzi kuliko yenye tija?

Kama ulivyoelekezwa hapo juu. Search engine huleta matokeo maarufu yaliyotafutwa sana na wewe, jamii yako, lugha uliyotumia na kifaa ulichotumia.

Hivyo lawama uanze kuzibeba wewe na jamii yako.
 
Sio google wameyapa kipaumbele,ila sisi tunaosearch ndio tunayasearch mara kwa mara ya kuyafanya yawe yanatangulia kutoka
 
Kuna kitu inaitwa SEO ni techniques ambazo zinatumika kuifanya blog/ web kiwe ranked on top, na mwandishi kama amezitumia kuna probability web yake ikawa juu. Pia Google ina track ni vitu gani watu wa eneo flani wana search sana. Ukiandika kitu obviously kama locality yako wengi wana search hivyo basi vitauwa displayed juu.
Halafu nachoona kikubwa hapo ni wewe hapo ndiye hujui kuwa specific ni nini unataka. Kuna jinsi ya kusearch kitu google ili ikuletee unachotaka specifically.
Huwezi kuandika vitu general general uka assume kuwa google itaelewa moja kwa moja unachotafuta. Mfano nataka kujua TANU ila naaka source iwe jamii forums basi nitaandika TANU "jamiiforums" na kusearch. Huo ni mfano mmoja na pia keywords unazotumia kusearch habari zako zinabidi ziwe specific
 
vinasachiwa sana so match engine za google zinatoa match case zinazotafutwa zaidi.Zinajua na wewe mshenzi wale wale
 
Hakuna kitu kama hicho.

Ukiona Google inakuletea mambo ya kipuuzi basi chanzo ni wewe sababu mara nyingi unatafuta hayo mambo ya kipuuzi.

Vilevile inaangalia eneo ulipo wanapendelea nini.

Hivyo ukiona umeandika vumbi na faster inakuletea vumbi la kongo basi tambua wewe kuna siku ulisearch vumbi la kongo kwenye search bar na hivyo google ikaona uko interested kwenye hilo vumbi.

Mradi una Gmail account au unatumia Google basi Google nakuwa inakuangalia siku zote na kuangalia kila unachofanya mtandaoni hivyo inajua nini unapenda kukifanya mara kwa mara na kukuletetea vitu unavyopendelea au unavyovipenda.

So mkuu hapa umejiexpose kwamba wewe ni mdau wa mambo ya kipuuzi hivyo Google haina makosa wala siri yoyote juu ya mambo ya kipuuzi.

A nikuulize wewe umejuaje kuhusu hayo mambo ya kipuuzi uliyoorodhesha?
 
Naomba uandike nabii kwenye search Google then U-screenshort majibu uweke hapa! Usijifanye mkristu kuliko waroma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…