Ipi tiba ya tatizo sugu la M'BA kwenye ngozi?

Ok,lakini hiyo aliyoonyesha hapo ni cream,nayo ni vipi...?
 
Ok,lakini hiyo aliyoonyesha hapo ni cream,nayo ni vipi...?
Nilijibu haraka haraka..

Cream haina shida ila inabidi asipake maeneo ambayo dawa inaweza kuingia kwenye mfumo wa damu..mfano maeneo karibu na macho.

Yenye shida sana ni vidonge vya kumeza.
 
Pole sana..nlikua nao nikahangaika miaka 10 ila nimekuja kuponea Kawe kwenye Dispensary moja ya masister ipo kawe mwisho wa kituo pembeni ya Jengo la NIDA.
 
Kwanza jitahidi kunywa dawa za minyoo kwa wakati, pili jitahidi unywe dawa ya kuharisha walau mara 2 kwa mwaka ili kuondoa sumu mwilini na kusafisha damu, fanya mazoezi, pia kuna sabuni za ubuyu anauza Shifaa yupo kariakoo nyuma ya kfc zinauzwa 1,000 tu ila ni nzuri mno utapendeza mpaka ujishangae mwenyewe
 
Mkuu, Hauhitaji kutumia gharama sana,
Tumia lotion moja inaitwa TOP LEMON, na hizi sabuni nyeusi RUNGU/FAMILY.
Hii lotion ukimaliza kuoga na hizo sabuni nilizotaja unapakaa tu kidogo eneo lililoathirika, kuwa na mwendelezo huo, baada ya week moja leta mrejesho

N.b Zingatia usafi wa nguo au ikibidi tumia pasi kabsa kutoruhusu mwendelezo wa masalia ya vimelea vilivyopo kwenye nguo zako pindi unapobadilisha.

Utanishukuru baadaye.
 
Naomba maelekezo kuhusu hizo dawa za kuharisha.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…