Ipo haja ya vinywa vya wahubiri kufungiwa speed governor?

Ipo haja ya vinywa vya wahubiri kufungiwa speed governor?

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Nimepita mahala muda sio mfupi na kumkuta mtumishi mmoja wa bwana akitoa mahubiri yenye ukakasi kwelikweli huku akishangiliwa kwelikweli na hadhara yake,nimemsikia kwa masikio yangu mawili eti akisema wanawake wa sasa hivi wamekuwa mercenaries

Hii ni sawa kweli kumfananisha mwanamke na Wagner group

Kwa sasa nimeondoka eneo la hayo mahubiri lakini nahisi mpaka mwisho wa mahubiri yake ataweza kuwafananisha wanawake na virus vya corona kwa sababu anaongea kama mtu mwenye hasira za kuachwa
 
kumbe Hawa watu wapo sehem nyingi?
hapanilipo Wana ratiba ya ibada kwa wiki Mara nne.kuanzia saambili asubuhi Hadi saa kumi jioni

tushazoea makelele sasa.mchungaji anajiita nabii
[emoji38]

Ova
 
Watu wananchezewa sana akili na majambazi ya dini za kuletewa. Jana tu nilikuwa sokoni Mabibo mida ya saa tisa mchana nakunywa supu ya mapupu na chapati zangi Mbili, akaja mwanamama mmoja mtu wa makamu kidogo akaanza kunihutubia neno la Mungu na kuniambia kwanini Mungu anataka watu wafunge mfungo wa Ramadhani. Nikamuomba yule Mama aniache akahubirie watu wengine wanaopenda kusikia mawaidha ya dini zisizo na mashiko, akanishangaa, nikamuuliza tena.....ni lini Mungu alimtuma yeye aje kwangu kuniambia kuwa kufunga ni lazima? Akanyamaza na kunishangaa kisha akaondoka zake. Hizi dini za kuletewa zina laana zake, unakuta mtu ana hasira toka nyumbani kwake, anapita mitaani kutafuta watu wanaokula aanze Kuji-Mungufy (Mungufai) na kutishia watu bila hata haibu.
 
Back
Top Bottom