Watu wananchezewa sana akili na majambazi ya dini za kuletewa. Jana tu nilikuwa sokoni Mabibo mida ya saa tisa mchana nakunywa supu ya mapupu na chapati zangi Mbili, akaja mwanamama mmoja mtu wa makamu kidogo akaanza kunihutubia neno la Mungu na kuniambia kwanini Mungu anataka watu wafunge mfungo wa Ramadhani. Nikamuomba yule Mama aniache akahubirie watu wengine wanaopenda kusikia mawaidha ya dini zisizo na mashiko, akanishangaa, nikamuuliza tena.....ni lini Mungu alimtuma yeye aje kwangu kuniambia kuwa kufunga ni lazima? Akanyamaza na kunishangaa kisha akaondoka zake. Hizi dini za kuletewa zina laana zake, unakuta mtu ana hasira toka nyumbani kwake, anapita mitaani kutafuta watu wanaokula aanze Kuji-Mungufy (Mungufai) na kutishia watu bila hata haibu.