Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
VITU USIVYOVIJUA KUHUSU SIKU MOJA.
1. Ipo siku utafunga mlango wako lakini utashindwa kuufungua.
2. Ipo siku utafua nguo zako lakini hutaweza kuzivaa
3. Ipo siku chakula kizuri kitapikwa lakini hutaweza kukila.
4. Ipo siku utakula na kunywa, lakini hutaweza kuvitoa chooni.
5. Ipo siku CV yako na uzoefu wako wa elimu havitakuwa na maana yoyote ile mbele ya mtu yeyote yule.
6. Ipo siku mtu anaekupenda, ataliita sana jina lako lakini hutaweza kuitika
7. Ipo siku utafikiri kitu ambacho hutaweza kukitenda.
8. Ipo siku majina yako yataongezeka.
9. Ipo siku watu unaowapenda na kuwakubali watakuja mbele yako lakini hutaweza kuongea nao kabisa.
10. Ipo siku utavuta hewa ndani ya mapafu yako lakini hutaweza kuitoa nje.
11. Ipo siku utalala kwenye ardhi na utafunikwa na udongo
12. Ipo siku utakuwa mtuhumiwa na kabla ya hakimu mkuu (Mungu) kukuhukumu.
13. Ipo siku nzi na wadudu watakuja mwilini mwako na hutaweza kuwafukuza
14. Ipo siku simu yako itapigwa lakini hutaweza kuipokea.
15. Ipo siku Mali na vitu ulivyovitafuta na kuvimiliki, vitamilikiwa na mtu mwingine.
16. Ipo siku habari zako zitasimuliwa katika wakati uliopita, watasema "alikuwepo". Hawatasema huyu ni mtu mzuri, bali watasema "alikuwa mtu mzuri"
17. Ipo siku hiyo ngozi yako nzuri itapukutika mithili ya ua linyaukalo jangwani.
18. Ipo siku picha yako nzuri kuliko zote itachaguliwa kukutambulisha kwenye umati wa watu
19. Ipo siku watu watakusanyika kukusindikiza sehemu ambayo utabaki mwenyewe.
20. Ipo siku hii simu uliyoishika, hutaweza kuishika tena. Na hata haya maandishi hutaweza kuyasoma tena kamwe.
IPO SIKU ..............
Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app