kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
...Tunatumia fedha nyingi sana zisizolingana na uwezo wetu kuwasomesha watu wachache, ili baadaye na wao walete faida kubwa kiasi hicho hicho katika nchi.
Tunatumia fedha kutafuta faida katika akili ya mwanadamu...tunatarajia mwanafunzi tuliyemsomesha chuo kikuu kutusaidia kiasi kikubwa zaidi katika kazi za maendeleo kuliko yule ambaye hakupata bahati hiyo. ..
Haya ni maneno Mwalimu Julius Nyerere aliyotamka tarehe 29 Februari 1968, kuhusu jukumu la wasomi kuindeleza nchi na jamii zao. Lakini je, hivyo ndivyo ilivyo?
Mlolongo wa matukio ya ufisadi na ubadhirifu wa mabilioni ya pesa za umma, kwa asilimia karibu 99 yamekuwa yakifanywa na wasomi.
Ripoti za Rada, Richmond, uuzwaji wa wanyama, kughushi malipo hewa, kampuni bandia, wizi Benki Kuu na mamia ya matukio ya wizi mkubwa wa mali ya umma unafanywa na wasomi.
Wananchi wa kawaida huko vijijini wametulia kimya wakiendeleza jitihada zao za kutafuta riziki kwa njia halali, huku wakibinywa na kodi na Serikali ili wasomi wanufaike.
Kuporomoka kwa uchumi wa nchi na hata kuanguka kwa elimu yetu, sababu kuu ni wasomi waliojivika sura tofauti tofauti kulingana na ofisi au mahali wanakofanyia kazi.
Uamuzi mwingi wa ovyo unaoivuruga nchi unafanywa na wasomi; wananchi wasio na digrii ndiyo wazalishaji na ndiyo wanyonywaji.
Tujikumbushe historia; miongoni mwa malengo makubwa ya wakoloni kutwaa bara la Afrika na kwingineko, ilikuwa ni kuiba rasilimali za maeneo hayo ambako wananchi walionekana wamelala.
Wakoloni walilenga kuvuruga mila na desturi ili jamii zisijitambue. Walipandikiza mitazamo ya kujidharau na kudharau kila cha Mwafrika, ubinafsi, choyo, chuki na umimi. Walitugombanisha, wakavuruga akili za wenyeji na mifumo asili ya uzalishaji.
Wenyeji wakatumika kama manamba na vibarua wa dezo kuzalisha malighafi walizozitaka. Kubwa zaidi, walituwekea mitazamo bandia, masomo bandia, mipango bandia ili tuhangaike nayo wakati wao wanaendeleza ubunifu,uvumbuzi, ugunduzi na sayansi ya hali ya juu. Je, kwa tafsiri ya Nyererena matendo ya wasomi kwa sasa tunaweza kutofautisha kati ya wasomi na wakoloni?
Malengo ya kusoma kwa sasa ni tofauti na mawazo ya Nyerere. Hata wasomi waliosoma enzi za Mwalimu Nyerere kwa kodi za wananchi, nao sasa ni bure!
Serikali chini ya Mwalimu iliwasomesha hadi ngámbo ikijua wasomi hawa watarudi na maarifa ya kutosha, watakuwa wabunifu, watakuwa na ujuzi na watawaongoza wenzao kwenye neema na siyo ufisadi na utapeli mkubwa uliopo sasa.
Hata hivyo, wengi wao waliosomeshwa na Serikali kwa pesa za umma, wamegeuka wezi wakubwa wa mali za umma. Nchi inaangamia bila majibu ya matatizo yetu. Kila anayepata fursa, anakula na kuivuna nchi; kisha kuiacha na umaskini wake. Inasikitisha kuona wasomi ambao wangekuwa mstari wa mbele kutafuta na kubuni njia za kutatua matatizo ya wananchi kwa kutumia maarifa waliyopata darasani, wao wanageuka mzigo mkubwa kwa taifa na wananchi.
Wengine tangu wapate digrii au u-profesa hatujawahi hata kuona kazi zao. Hata mtaa wanaokoishi haufaidiki lolote na usomi wao. Wamebaki kutamani vyeo vikubwa tu, mishahara mikubwa tu, posho kubwa, ofisi kubwa na starehe kubwa. Ni mzigo kwa taifa!
Jamii inajitahidi kulipa kodi ambazozinakwenda kulisha wasomi hawa waliojipenyeza kwenye taasisi nyetiza Serikali, huku wakigawana posho kwa kukaa tu kwenye viti vyakuzunguka na kwenda Ulaya kutalii,huku kodi za Watanzania zikifujwa kwenye hoteli kubwa huko Ulaya naMarekani.
Kwa sasa ukisoma hurudi hata kijijini ulikozaliwa. Hata majina ya Kiafrika yanabadilishwa, ili waitwe majina kizungu, wakae mijini kwenye fursa za kupora na starehe lukuki.
Ndugu zetu vijijini wanabaki hawana msaada wa kimawazo, kila msomi ni wa mjini na Ulaya. Wanajifungia tu ofisini huku wakicheza michezo ya kwenye kompyuta na kusoma barua pepe. Siku inaisha; mwisho wa mwezi wanadai mishahara mikubwa.
Wapo walio kwenye siasa na kuwa mawaziri, wabunge lakini wako huko kwa minajili ya kushibisha matumbo yao tu. Hawazijui hata sera wanazozimamia na kuziimba majukwaani.
Siku zote wanapenda kuitwa waheshimiwa, huku uheshimwa wao hauonekani. Na kwa sasa wanalipwa posho kwa kutukanana na kuonyesha umahiri wa ngebe na kejeli bungeni.
Nilishawahi kuandika kuwa wapo maprofesa wetu wamesomea uhandishi wa madaraja, lakini hawawezi hata kujenga daraja la kupita kuku wake nyumbani.
Wachina wanavuna mabilioni ya pesa nchini mwetu kwa kujenga majengo, barabara, mitambo na kilakitu kizuri kwa elimu ya VETA tu, huku sisi wasomi tukiendelea kuwatukana kuwa wanatengeneza vitu feki. Wanarudi kwao na utajiri mkubwa, kweli wajinga ndiyo waliwao! Pia wapo baadhi ya wasomi ambao wanajiita wataalamu wa tafiti na hata wengine kujiita wanaharakati wa haki za binadamu.
Kweli wapo wachache makini sana na wanachapa kazi, lakini wengi ni wababaishaji tu walioanzisha asasi za mifukoni zisizo na kichwa wala miguu.
Wamegeuka vibaraka wa wazungu wanaowatumia kuharibu mila na desturi za Waafrika kwa kutoa mafundisho potofu yanayozitukana mila zetu na kuukumbatia uzungu uliojaa uchoyo, ubinafsi na wizi.
Kwa sababu wanapatiwa pesa na wazungu, kampeni zao za kuangamiza watoto wetu zinaonekana kila siku kwenye vyombo vya habari.
CHANZO: MWANANCHI