Haya ni uzembe kwenye internet website, lakini pia Kumekuwa na mazoea ya makosa mengi tu IPP Media print, mpaka imefika kwamba ukiona kosa wala hushangai, lakini unajiuliza Editors walikuwa wapi.
Labda ni ile kwamba tumejenga tabia ya mwandishi kuridhika na kitu alichokiandika bila kukisoma mara kadhi ili kuondoa vimakosa vidogovodogo ambavyo vinapunguza umahiri wa mwandishi na Editor wake.
Ukiangalia hata staili ya kuandika inasikitisha kiasi fulani, kwani huonyesha kazi ya kulipua boara nimeandika. Mara kadha mimi badohuona kipande cha gazeti kama Times la miaka kadha nyuma, bado unaona raha kulisoma unafurahia ile "presentation" tu japo habari imepitwa na wakati, unafurahia "grammar, planning, humour na analysis" kwani inafundisha kitu fulani. Labda ningewashauri hawa waandishi wetu kuwa wanasoma vya wenzao, sio kupata habari tu, bali kujifunza namna ya kuandika na kuvutia wasomaji.