mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,904
- 8,371
Huko Kenya kampuni kubwa ya Utafiti Ipsos imeingia kwenye mgogoro mkubwa na Makamu Raisi wa Kenya Mheshimiwa sana William Ruto,kutokana na utafiti waliofanya ,wananchi wengi wamedai Ruto na Anne Waiguru ndio viongozi wanaongoza kwa kula rushwa,habari hii haijakuwa nzuri kwa Ruto na timu yake,na sasa Ipsos imekuwa ikipewa majina mabalimbali na wapambe wa Ruto na kudaiwa tafiti zao ni za kupikwa au zinafadhiliwa na wapinzani wa Ruto kwa ajili ya kumvurugia njia ya kuelekea uraisi.Nikiangalia hizi sarakasi za viongozi wa kiafrika kupinga hizi Opinion Polls pale zinapoenda kinyume cha matarajio yao huwa zinaniacha hoi.Nadhani viongozi wengi ama hawajui maana ya Opinion Polls au basi wanataka wasifiwe tu. Siku hizi kufanya Opinion Polls kwenye nchi za Kiafrika ni kutafuta ubaya kwa mamlaka zilizopo,nadhani sasa Opinion Polls zimekuwa ndio sauti ya wasio na sauti,si ajabu kwa sasa kupata vibali vya kufanya Opinion Polls nchi za Kiafrika ni sawa na NGAMIA KUINGIA KWENYE TUNDU LA SINDANO