Ipsos Kenya yaleta kizazaa ,kisa maoni yasema Ruto ni mla rushwa mkubwa

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,904
Reaction score
8,371
Huko Kenya kampuni kubwa ya Utafiti Ipsos imeingia kwenye mgogoro mkubwa na Makamu Raisi wa Kenya Mheshimiwa sana William Ruto,kutokana na utafiti waliofanya ,wananchi wengi wamedai Ruto na Anne Waiguru ndio viongozi wanaongoza kwa kula rushwa,habari hii haijakuwa nzuri kwa Ruto na timu yake,na sasa Ipsos imekuwa ikipewa majina mabalimbali na wapambe wa Ruto na kudaiwa tafiti zao ni za kupikwa au zinafadhiliwa na wapinzani wa Ruto kwa ajili ya kumvurugia njia ya kuelekea uraisi.Nikiangalia hizi sarakasi za viongozi wa kiafrika kupinga hizi Opinion Polls pale zinapoenda kinyume cha matarajio yao huwa zinaniacha hoi.Nadhani viongozi wengi ama hawajui maana ya Opinion Polls au basi wanataka wasifiwe tu. Siku hizi kufanya Opinion Polls kwenye nchi za Kiafrika ni kutafuta ubaya kwa mamlaka zilizopo,nadhani sasa Opinion Polls zimekuwa ndio sauti ya wasio na sauti,si ajabu kwa sasa kupata vibali vya kufanya Opinion Polls nchi za Kiafrika ni sawa na NGAMIA KUINGIA KWENYE TUNDU LA SINDANO
 
Dhambi ya kutaka kusifiwa bila kukosolewa kwa viongozi wetu inarudisha bara hili nyuma kimaendeleo. Kiongozi sio mungu kwamba hawezi kukosea! Wakubali kupokea maoni tofauti ili tusonge mbele!
 
Kumbe ni kweli Kenya wako tofauti sana na sisi. Utafiti wa IPSOS unasema Ruto ni mlarushwa. Wanaopinga ni Ruto na wapambe wake. Hatujaona Polisi, Uhamiaji wala Usalama wa Taifa kuwakamata viongozi wa IPSOS kwa vile ulaji rushwa ni tabia binafsi ya Ruto hivyo anatakiwa kubeba mzigo wake mwenyewe. Huku kwetu sasa wee! Umaarufu wa Magufuli umeshuka toka 95% hadi 54%(TWAWEZA). Vyombo vyote vya serikali midomo juu utafikiri umaarufu binafsi wa Magufuli ni suala la kitaifa!! Hivi umaarufu nayo ni sehemu ya utendaji wa Rais na una faida gani kwa wananchi wa kawaida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…