kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la IRGC alionya jeshi la Marekani katika Ghuba ya Uajemi
May 29, 2023 02:31 UTC
[https://media]Alireza Tangsiri
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) amepinga vikali kuwepo kwa jeshi la Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi kwa kisingizio cha kulilinda eneo hilo la kistratijia la baharini.
Meja Jenerali Alireza Tangsiri amesema kwamba Iran na nchi nyingine za kieneo pekee ndizo zitakazohakikisha usalama wa Ghuba ya Uajemi na hakuna haja ya Marekani na nchi nyingine ajinabi kuwepo katika njia hiyo ya kistratijia ya majini.
"Mumekosea sana kuwepo katika eneo letu," Tangsiri amesisitiza na kusema: "Hatuna chaguo jingine isipokuwa kusimama na kupambana, na hii ndiyo njia ya ushindi wa taifa letu."
Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la IRGC aliyasema hayo katika hafla rasmi iliyofanyika kwenye mji wa Dezful katika mkoa wa Khuzestan, Kusini-Magharibi mwa Iran, ambapo alipongeza mapambano ya kustaajabisha yaliyofanyika katika mji huo wakati wa uvamizi wa Iraqi katika miaka ya 1980.
Akiitaja Dezful kama nembo ya mapambano na kusimama ngangari, Tangsiri amesema: "Katika miaka minane ya Kujitetea Kutakatifu (vita vya Iran na Iraq), tuliuonyesha ulimwengu kwamba hatukujisalimisha na hatutasalimu amri."
Amesisitiza kuwa: "Tunasimama kidete dhidi ya adui na tutalinda heshima na hadhi ya taifa la Iran."
Iran imeweka wazi kuwa inaziona meli za kijeshi za Marekani katika maji ya Ghuba ya Uajemi kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa lake na chanzo cha mivutano na ukosefu wa utulivu katika eneo hilo.