Irene Uwoya aacha kuigiza!

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,285
Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.
Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”
Ireneambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.
Ni show ambayo haitahusika kujenga nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama za mamilioni kwa kutegemea ubovu wa nyumba yenyewe, ambapo Irene amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho cha pesa kama bajeti ya kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati nyumba ikamilike.
Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.
Show yake ya TV imeshaanza kuonekana Tanzaniapamoja na kupata wadhamini ambao watamuwezesha kwenye kazi hii kubwa ya kupokea maombi ya Watanzania mbalimbali ambao wanahitaji nyumba zao zirekebishwe bure, kupitia kipindi hicho cha TV.
Show kama hii ambae inaitwaExtreme Makeover: Home Editioninapatikana kwenyeBBC Lifestyle ikiletwa kwako kila siku saa 18:10 CAT.

Source! http://www.dstv.com/News/Irene-Uwoya-kaacha-kuigiza/28435
 
Inaoneshwa bbc? Hapo mzee wa bamaga atamfuata hadi huko ili amchafue tena
 
wasanii wa bongo hasa wa tasnia ya filamu, elimu HATUNA KABISAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! si ya sanaa wala hii ya kawaida!!

angekuwa na elimu huyo asingepata shida hata kidogo na wala shigongo asingeweza kumuendesha!!
 
Maskini we kwanini kaacha kuigiza?
 
Watu mnasoma kwa kukurupuka, sijui mnasoma huku mnakimbizwa, au mnasoma huku mmebanwa na haja ( haja kubwa ndo ina tabia hizi)

Kuna show kama hii ambayo inaonyeshwa BBC. Watu mmeelewa show hii inaonyeshwa BBC...mmebanwa na haja sio bure
 
...Umeniwahi! Nilikuwa niishavuta 'ukurasa' kuandika hivi hivi ambavyo umeandika! Asante. Yaani watu hawaitendei kabisa Haki JF kwa kukurupuka...!:A S 39:
 
Watu mnasoma kwa kukurupuka, sijui mnasoma huku mnakimbizwa, au mnasoma huku mmebanwa na haja ( haja kubwa ndo ina tabia hizi)

Kuna show kama hii ambayo inaonyeshwa BBC. Watu mmeelewa show hii inaonyeshwa BBC...mmebanwa na haja sio bure

what a fnck!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…