Irene Uwoya: Sitaki Mwanangu Alale kwa Ndugu!

Irene anajaribu kuwakwepa wale mafundi wa kutafuta KIPENYO CHA DUARA

Unaambiwa mzingo wa Duara n sm 154 tafuta KIPENYO sasa hapo hamna rangi ataacha kuiona

ASISAHAU MJOMBA NI MAMA
 
Kulala kwa ndugu kunaingilianaje na kuiaribika kwa mtoto. Mtoto hata umfungie ndan au umbebeshe bibilia na quran kila mda kama ni wa kuharibika ni wa kuharibika tu. Tatizo kama amejua mandugu zake ndo shida kwa nini asiwakalishe chini awaambie waache hiyo tabia itakayoharibu mtoto wake. Acha tu ninyamaze maana...
 
Unaogopa ataliwa?wewe mbona unawakula wengine
 
Ukiona mambo yako yanakwenda vizuri, una kazi nzuri, una familia bora, watoto wanafanikiwa, kifupi umejipata, usidhani wewe una kunywa chai na Mungu. Ni kwa neema tuu. Wale wasio kama wewe usiwaona kama wamepoteza ramani kwenye maisha au wanakosea mipango. Wala ukiona wanao wanafanikiwa usidhani wewe ndo mzazi bora.

Bustani inaweza kuwa moja lakini kila mti hutoa maua kwa wakati wake.
 
Mkuu naamini una watoto. Kama huna una ndugu wenye watoto. Kuwa mchache wa kuhukumu. Maisha yana mengi.
Ww ukimungalia huyo mtoto, yupo sawa na watoto wa kiume mtaani kwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…