Irene uwoya yupo hatarini sana kupoteza ubunge viti maalum

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
View attachment 276421
muigizaji wa bongo movies Irene Uwoya aliyejiunga na ccm na kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalum tabora yupo hatarini kupoteza cheo chake cha ubunge wa viti maalum na huenda wabunge viti maalum wengi sana wa ccm nao wataachia ngazi.

mbunge viti maalum aliechaguliwa kwa sasa ataingia mjengoni mpaka ifikapo oktoba baad ya kampeni na uchaguzi ambapo kila
jimbo litapata mbunge(sio wa viti maalum) wake ambapo hawa wabunge wa viti maalum waliochaguliwa saizi italazimu idadi yao ilingane sawa na idadi ya wabunge wawakilishi wa majimbo wa vyama vyao, mfano kwa ccm mwaka 2010 kabla ya kampeni walikuwa na wabunge viti maalum 92 ila baada ya kampeni na uchaguzi ilipata wabunge 60, kutokana na kupoteza majimbo mengi hivyo ikabidi idadi ya wabunge wa ccm wa viti maalum ipungue toka 92 hadi 60, na wakati wao ccm waliandaa wabunge 92 wa viti maalum wakijua watapata majimbo mengi , matokeo yake ikabidi chama kiwapunguze hadi 60 na baada ya hapo nafas zilizobsaki 22 za wabunge viti maalum wakapewa chadema.

Kwa sasa ni wazi kabisa tembo yupo shambani ambayeaneyejifanya hamuoni aende mahututi, kwa upepo huu wa siasa
ni wazi kabisa ukawa, act na vyama vingine watachukua majimbo mengi sana kwenye nafasi za ubunge(sio ule wa viti maalum), hivy basi endapo CCM itapata wabunge kwenye majimbo machache asilimia hiyo ya wabunge itabidi ilingane na wabungewataopitishwa kwenda kuwakilisha majimbo kwa nafasi za viti maalum na kukilazimu chama kukata wabunge viti maalum wawe wachache
 
Hawezi kupoteza kitu ambacho hana.
Huyu siyo mbunge, hivyo hawezi kupoteza Ubunge.
Hivyo nakushauri ukamshauri kuwa asihofu kabisa kwa maana hana cha kupoteza.
 
Hawezi kupoteza kitu ambacho hana.
Huyu siyo mbunge, hivyo hawezi kupoteza Ubunge.
Hivyo nakushauri ukamshauri kuwa asihofu kabisa kwa maana hana cha kupoteza.

Well said
 
Huyu naye mbunge...mbona hawachagui wavuta bangi? Wanawachagua wagawa pachuchu tu...
 
Hawezi kupoteza kitu ambacho hana.
Huyu siyo mbunge, hivyo hawezi kupoteza Ubunge.
Hivyo nakushauri ukamshauri kuwa asihofu kabisa kwa maana hana cha kupoteza.

ila kwa sasa ni mbunge viti maalum mtarajiwa endapo ccm kwa bahati labda ikoshinda majimbo mengi
 
ila kwa sasa ni mbunge viti maalum mtarajiwa endapo ccm kwa bahati labda ikoshinda majimbo mengi

Na hyo bahati haipo labda asubirie 2020 kama atakua hai bado
 
Hata mi nahisi hivyooo akipata bahati sana
 
Kwa hiyo ccm wakipoteza majimbo mengi uwoya ndio atakayeenguliwa?? Sina mapenzi na huyo uwoya ila nahisi hoja yako ni ya kitoto na hukutumia akili yako sawa sawa kuiwakilisha?? Kwanini umtaje yeye wakati kuna maboksi mengine kibao?? Ugomvi wenu wa kwenye sinema msituletee huku
 
Anawakilisha kundi gani huyo mtu? Au kuna mkakati wa kuhalalisha biashara ya kona bar ndio huyu mwakilishi wao anakwenda kuwapigia chepuo?
 
Anawakilisha kundi gani huyo mtu? Au kuna mkakati wa kuhalalisha biashara ya kona bar ndio huyu mwakilishi wao anakwenda kuwapigia chepuo?

Inawezekana Biashara ya kona bar ikahalalishwa na huyo akawa mwakilishi wao
 
Inawezekana Biashara ya kona bar ikahalalishwa na huyo akawa mwakilishi wao
Aiiiisee kama ni hivo poa na wenyewe wamepata mwakilishi ni biashara inayopigwa vita sana japo sisi wakina madomo zege na tusiopenda kupotezeana muda inatusaidia sana.
 
mmmmh mie napita,
hivi kwani unatakiwa kuwa na sifa zipi ili uwe mbunge viti maalum?
na huwa kazi yao kuu ni ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…