Pre GE2025 Iringa: Kuna ongezeko la vituo 140 vya uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Pre GE2025 Iringa: Kuna ongezeko la vituo 140 vya uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Kuelekea kuanza kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura Mkoani Iringa imeelezwa kuwa kuna vituo vipya vipatavyo 140 vimeongezwa.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 15, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mtibora Seleman katika Mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi Mkoani Iringa, imeeleza kuwa vituo vitavyotumika katika uandikishaji ni 1,367 sawa na ongezeko la vituo 140 ukilinganisha na idadi ya vituo mwaka 2019/20 ambapo kulikuwa na vituo 1,227.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa zilizopo Manispaa ya Iringa chini ya uangalizi wa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mbarouk Mbarouk.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura Mkoani Iringa linatarajiwa kuanza Desemba 27 na kufika tamati Januari mbili mwaka 2025 huku likiongozwa na kauli mbiu ya "Kujiandikisha kuwa Mpiga ni Msingi wa Uchaguzi Bora"

Screenshot_20241215-233332.jpg
 
Back
Top Bottom