Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, amepongeza mwenendo wa upigaji kura katika mkoa huo, akieleza kuwa mchakato huo umekwenda vizuri licha ya baadhi ya changamoto zilizojitokeza. Serukamba amesema changamoto hizo zimeshughulikiwa haraka ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na haki.
Serukamba amesema hayo Novemba 27, 2024 mara baada ya kupiga kura katika mtaa wake wa Shule ya Msingi Gangilonga mkoani humo, ambapo aliwataka wananchi kuendelea kujitokeza kupiga kura kwani ni haki yao ya kikatiba.